Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
leo anatarajiwa kuzindua rasmi shughuli za bunge la kitaifa kuhusu
marekebisho ya katiba mjini Dodoma katika hatua itakayoanzisha rasmi
mjadala wa kitaifa kuhusu marekebisho hayo.
Bunge hilo maalum la katiba limepewa kati ya
siku 70 hadi 90 kujadili rasimu ya katiba na kisha kuifanyia marekebisho
kabla ya kura ya maamuzi.Suala la hotuba ya Rais Kikwete limekuwa sehemu ya mjadala katika Bunge hilo kutokana na baadhi ya wajumbe kuhoji sababu za Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu kabla ya Rais kuzindua Bunge kwa mujibu wa kanuni.
Mjadala huo uliwafanya baadhi ya wajumbe kumzuia Jaji Warioba Jumatatu iliyopita kuwasilisha rasimu hiyo kama ilivyokuwa imepangwa.
Kikao cha maridhiano kilifanyika siku hiyohiyo usiku na kufikia mwafaka kwamba Mwenyekiti huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe Rasimu ndiposa Rais aweze kuzindua shughuli ya kujadili rasimu hiyo kabla ya kura ya maoni.
No comments:
Post a Comment