Wednesday, March 12, 2014

MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGE LA KATIBA


Dodoma, Tanzania. Mchungaji Christopher Mtikila amechafua hali ya hewa bungeni, hivi punde kwa kumtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Kificho amueleze ni kwanini tangu jana amekuw akimnyima nafasi ya kuzungumza bungeni.

Mchungaji Mtikila alisimama ghafla na kusema: Mwenyekiti kwanini unaninyima haki yangu ya kuzungumza, nataka kujua kwanini unaninyima haki ya kuzungumza. Kuzungumza ni haki yangu."


Mchungaji Mtikila amezungumza kwa jazba huku wajumbe wengine wakimzomea, lakini bila uwoga aliendelea kuzungumza na kusema yanayofanyika Mungu anapenda na yeye ana amini katika Mungu, lakini "Wewe Mwenyekiti inaonekana kuwa hupendi Mungu."

Wakati Mchungaji Mtikila akimwakia Kificho, Felix Mkosamali alilipuka na kumwambia mwenyekiti kuwa tangu jana pia anamnyima nafasi.
"Ninyi mmejipanga, kupitisha kanuni mbovu, alafu sisi wengine hamtupi nafasi," amesema Mkosamali.

Mwenyekiti Kificho aliwajibu kuwa kwa bahati mbaya wamekosa nafasi na hivyo wawe wavumilivu.

Kificho anatangaza utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge na wajumbe wanaotaka kugombea nafasi hiyo wametakiwa kuchukua fomu ya kugombea.

Bunge hilo limeahirishwa mpaka kesho na kanuni zitaanza kufanya kazi rasmi.

No comments:

Post a Comment