Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka nje ya hoteli katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Polisi wanasema watu wanne wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.Maafisa wa serikali walikuwa ndani ya hoteli wakati wa shambulizi hilo.
Msemaji wa serikali amesema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab kama jibu lao kwa operesheni mpya iliyozinduliwa juzi na wanajeshi wa Muungano wa Afrika pamoja na majeshi ya Somalia dhidi ya wanamgambo hao.
Wanajeshi hao wamefanikiwa kukomboa miji sita kutoka kwa Al Shabaab katika siku chache zilizopita. Kundi hilo linadhibiti sehemu kubwa ya Kusini na eneo la Kati mwa Somalia.
No comments:
Post a Comment