Msanii
wa muziki wa Kizazi kipya Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa kuanza rasmi utaratibu wa
kugawana mirabaa na watengenezaji na wasimamizi wa kazi zake za sanaa.
Maamuzi
haya yamekuja chini ya mkataba mpya ambao CPwaa ameingia na "Record
label" yake ya "Brainstormusic" ambayo itazinduliwa rasmi siku
za usoni.Maamuzi haya ni magumu kwa wasanii wengi lakini kwa wale wafuatiliaji
na wadau wa muziki hakika wanatambua biashara ya muziki inafanyikaje na jinsi
kila muhusika anavyotakiwa kupata share zake kutokana na makubaliano
yaliyofikiwa na pande zote kupitia sheria za kitaifa na kimataifa za haki
miliki.
CPwaa
ambaye amakuwa akifanya kazi na "Brainstormusic" kwa miaka mingi
tayari amekuwa na mafanikio makubwa kimuziki kupitia uongozi na usimamizi wa
kampuni hiyo.Ukiacha tuzo 3 za Kilimanjaro Muisc awards,nomination za tuzo za
kimataifa kama Channel O ,CPwaa anaendelea kufaidika kupitia mikataba mizuri ya
shows na endorsements kwenye makampuni mbalimbali kupitia label hiyo.
.."Kupitia
Brainstormusic nimejifunza vitu vingi sana kuhusu sanaa ya muziki baadaa
kufanya kazi na makampuni ya hapa Tanzania na nje.Nimesafiri nchi nyingi Africa
na Asia kupitia muziki na kusema ukweli Tanzania kuna mambo mengi sana bado
hayako sawa kwenye biashara ya muziki" Umefika muda wa sasa kushare
experience na knowledge na kama tukifata utaratibu huu hakuna mtu atadhulumiwa
wala kulalamika.Kila mdau anahusika.".....aliongezea CPwaa!!
Kwenye
utayarishaji wa muziki kila muhusika huwa anakuwa kiwango fulani cha asilimia
ya mapato anapata kutokana na mchango wake.Kwa kawaida mapato ya muziki
"Royalties" hugawanywa kati ya Songwriter ( mtunzi wa nyimbo ambae
ndio mmliki halali wa nyimbo), Producer ( Mtayarishaji), Performing Artist (
Muimbaji wa nyimbo) na Publisher au Record label ( wasambazaji na wasimamizi).
Mgawanyo unatokana na kiwango cha mchango wa kila muhusika na mara nyingi huwa
makubaliano kati ya wahusika. Kimataifa au kawaida mtunzi huchukua asilimia
kubwa na wengine hupata sehemu tu mirabaa itakayokusanywa.Serikali haihusiki na
makubaliano ya asilimia za mirabaa kati ya wahusika au hatua za awali za hiyo
sanaa ila inahusika kwenye kuweka na kutoza kiwango fulani kinacholipwa na
vyombo vyote vinavyotumia kazi za sanaa na kisha kugawa mirabaa kwa wale
wamiliki wa hizo sanaa.
Kuanzia
mwaka huu Producer yeyote atakayefanya kazi na CPwaa chini ya usimamizi wa
"Brainstormusic" basi atafaidika si tu kwenye malipo ya awali ya
utengenezaji wa beat na studio time ila pia asilimia fulani ya mapatao ya
mirabaa itakayoingizwa na kazi hiyo. Kimataifa producer huchukua kati ya 20 -
25% kutokana na kwamba yeye kama mtengenezaji wa beat basi ndio mmliki wa ile
beat.
Huu
ni utaratibu mpya utakuwepo kwa maproducer wote watakaofanya kazi na CPwaa au
Brainstormusic kuanzia mwaka huu:
1.Kazi
zote zitaandaliwa na kufanywa chini ya makubaliano yaliyoandikwa na kusainiwa
na pande zote.Invoice na risiti zitahusika.
2.Brainstormusic
ikinunua beat pamoja na haki miliki zake ( yaani producer akiuza beat jumla)
basi hatapata share za mirabaa.
3.Kama
Brainstormusic au Msanii wake atahusika kwenye hatua za utayarishaji
beat,vionjo,idea,upangiliaji basi asilimia fulani ( Chini ya makubaliano) ya
mirabaa itatolewa na Brainstormusic kwa Producer wa kazi hiyo.
4.Kama
producer atahusika mwanzo mwisho kutengeneza na kukamilisha beat hiyo bila
uhusika wa Brainstormusic au msanii wake basi producer atapata asilimia fulani
kubwa zaidi ( Chini ya makubaliano) ya mapato ya mirabaa ya kazi hiyo.
5.
Ukiacha mapato ya mirabaa Brainstormusic itamlipa Producer au Studio gharama za
kawaida ( Delivery / Studio Fee) kama utaratibu ulivyo sasa.
Brainstormusic
ni Record label ya kujitegemea inayofanya kazi na wasanii,maproducers na makampuni
mbalimbali.Mwaka huu imedhamiria kujitanua kwenye Music Publishing hivyo
kupitia mikataba yake itahakikisha producer analipwa asilimia yake kutoka
makampuni mbalimbali kama ikiwemo Music Stores,makampuni ya milio ya simu na
PROs ( Performance Rights Organization) kama COSOTA.
Bado
hakuna utaratibu mzuri nchini Tanzania unaotumika kwenye utendaji na usimamizi
wa kazi za sanaa kuanzia hatua za awali."Brainstormusic" tunatambua
mchango na kuheshimu kila mtu kwenye "Food Chain" ya sanaa na hivyo
tutafanya kazi kufuata miongozo ya kitaifa na kimataifa ambapo kila mtu anapata
maslahi kutokana na mchango wake. Utaratibu huu hautaishia kwa CPwaa tu bali
wasanii wote watakaokuwa wakisimamiwa na "Brainstormusic".
No comments:
Post a Comment