Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema
hana mpango wa kuwahoji Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaotokana
na chama hicho kwa sababu ya misimamo yao inayokinzana na miongozo ya
chama, kwa kuwa anawafahamu wote kwa majina na idadi yao haizidi kumi.
Kauli hiyo ya Kinana inafuatia taarifa zilizoripotiwa na gazeti hili
hivi karibuni kuwa, CCM kimeanza kuwahoji baadhi ya wabunge wake, ambao
ni Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu ya kupingana na
maelekezo ya chama hicho kuhusu Muundo wa Serikali mbili.
“Sisi (CCM) hatuhoji mtu kwa sababu ya kuwa na msimamo tofauti, kwani
hawa wenye msimamo tofauti na chama hawazidi kumi ama siyo zaidi ya 15,”
alisema Kinana na kuongeza;
“Hawa watu mimi nawajua kwa majina, mmoja (jina tunalo) ni hatari zaidi
kwa sababu anaweza kuwakusanya wengine na kuwashawishi wafuate msimamo
wake, lakini waliobaki wote, hawatishi kwa kuwa wanabaki na misimamo yao
wenyewe.”
Kwa mujibu wa habari hiyo, wajumbe waliohojiwa ni wale wanaotokana na
Ubunge wa Jamhuri ya Muungano na ambao wanataka Muundo wa Serikali tatu.
“Ni kweli hata mimi niliitwa na akaniambia (mwakilishi wa chama)
ametumwa aniletee ujumbe kuwa niko kwenye orodha ya watu 90 na
nikiendelea na msimamo wangu nitachukuliwa hatua,” alieleza mmoja wa
wajumbe waliodai kuwa wamehojiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
Maelezo ya Kinana
Kinana aliliambia gazeti hili kuwa, kulingana na muundo wa chama hicho
tawala, viongozi wanaoweza kuwahoji watu ni yeye Katibu Mkuu, Makamu
Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa
chama Taifa. “Tena tunafanya hivyo kwenye vikao maalumu na kwa sababu
ambazo haziwezi kuwa siri.”
Kinana alieleza kuwa taarifa kwamba CCM imewahoji watu 90 kutokana na
kuwa na misimamo tofauti na chama hicho kuhusu Serikali mbili na kura ya
wazi, siyo za kweli na anaamini imesambazwa na watu kwa malengo yao
binafsi. Kinana anafafanua kuwa CCM kama chama kikubwa nchini chenye
wafuasi karibu nchi nzima, hakiwezi kudhibiti mitizamo ya watu na
kimsingi tofauti za mitazamo ndiyo msingi wa demokrasia.
Novemba 20 mwaka 2012 akizungumza katika kipindi cha Jenerali on Monday
kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Kinana alitoa
onyo kwa makada wasaliti kuwa atasimamia utekelezaji wa uamuzi wa
Halmashuari Kuu ya CCM (Nec) ya kuwabaini na kuwaondoa viongozi
wanaokwenda kinyume na matakwa ya chama na kukipaka matope.
Kura ya wazi na Serikali mbili
Katika hatua nyingine, Kinana alizungumzia msimamo wa chama hicho wa
kura ya siri na muundo wa Serikali mbili, akieleza kuwa siyo jambo la
ajabu, kwani katika mchakato wa kutunga katiba, kila kundi lina maoni na
mtazamo wake na kuutetea kwenye mijadala.
“Wanaosema kuna vyama havina msimamo pale bungeni ni waongo. Siyo vyama
tu, kila kikundi kina msimamo unaotokana na uchambuzi wao wa hali ya
siasa nchini na wanachofikiri kina masilahi kwa nchi na watu wanaofuata
mtazamo wao. Hawawezi kuniambia kama Lipumba (Profesa Ibrahim) na Mbowe
(Freeman), hawana wanachosimamia kwenye mjadala huo wa Bunge Maalumu,”
alisema na kusisitiza:
No comments:
Post a Comment