Saturday, March 15, 2014

Dondoo za ligi kuu ya Premier


Klabu ya Manchester City, imejifaidi nafasi ya kumsajili mchezaji wa miaka 16 Feyenoord Rodney Kongolo kiungo cha kati, ambaye amelingishwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira.

Liverpool wako makini kutaka kumsajili mlinzi wa Barcelona Adriano,mwenye umri wa miaka 29, kwa kima cha pauni milioni 6 wakinuia kukomesha masaibu yao.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anadhani kuwa difenda Ryan Bertrand, mwenye umri wa miaka 24,bado ana mustakabali mwema Stamford Bridge licha ya kusajiliwa na Aston Villa kwa mkopo.

Tottenham Hotspur wanatafuta njia ya kusajili wachezaji mahiri watatu msimu huu hasa baada ya baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni kutofurahisha meneja. Klabu hiyo ilitumia pauni milioni 110 kusajili wachezaji saba wakiwemo Erik Lamela, Roberto Soldado, Paulinho,Étienne Capoue, Nacer Chadli na Vlad Chiriches. Mustakabili wa wachezaji hao katika klabu hiyo unasuasua.

Adebayor
Mshambulizi wa Tottenham Emmanuel Adebayor, mwenye umri wa miaka 30, anasema kuwa hatataka msukumo wowote atakaposhiriki mechi dhidi ya klabu yake ya zamani Arsenal Jumapili. Mchezaji huyo mzaliwa wa Togo alichezea Arsenal kwa miaka mitatu kati ya mwaka 2006 na 2009.

Mshambulizi wa New Castle Luuk de Jong, 23, ana matumaini ya kupata mkataba wa kudumu ,St James' Park wakati kipindi chake cha usajili kwa mkopo kitakapokwisha katika klabu ya Ujerumani Borussia Monchengladbach mwishoni mwa wiki hii.

Chelsea imejiimarisha baada ya kusaini mkataba na mchezaji Raia wa Brazil Hulk mwenye umri wa miaka 27 baada ya wakala mmoja kufichua kuwa mchezaji huyo wa Zenit ananuia kuhamia Uingereza.

No comments:

Post a Comment