Maafisa wa utawala katika
Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo wametangaza siku tatu kuomboleza
wakimbizi waliofariki katika ajali ya boti katika ziwa Albert siku ya
Jumamosi.
Boti hiyo, ilikuwa inawasafirisha wakimbizi wa DRC kutoka nchini Uganda wakirejea nchini mwao.Inaarifiwa boti hiyo ilikuwa imebeba abiria zaidi ya inavyoweza kumudu na maafisa wanasema kuwa zaidi ya watu miambili hamsini waliOkuwa wameabiri boti hiyo walizama.
Serikali ya Uganda ilisema kuwa iliweza kupata maiti 107 ikiwemo watoto 57 baada ya bnoti hiyo kuzama. Wote walikuwa wanatarajiwa kufika salama nyumbani DRC.
Walikuwa wanaishi katika kambi za wakimbizi nchini Uganda na inaarifiwa watu 300 walikuwa wameabiri boti hiyo illipozama.
No comments:
Post a Comment