“Yaani mto huu ni tishio kubwa kwa wapita njia kwani unaweza kuwa eneo lako mvua haijanyesha ukajiamini kwa kupita lakini kama imenyesha eneo lingine ukashangaa maji yamejaa ambayo yanao uwezo wa kumeza mtu, hili ni tatizo na mbaya zaidi unapanuliwa na wachimba mchanga” alisema mama Mmoja anayefahamika kwa jina la Mama Adelina.
Aidha wakazi wa huko wametoa kilio chao kwa serikali kuwatengenezea daraja kwa ajili ya kuvuka wakati wa mvua kwani ardhi ya huko kupita njia nyingine imekuwa haifai kabisa kwasababu ya mfinyanzi hasa wakati wa mvua tatizo ambalo ni la muda mrefu.
No comments:
Post a Comment