Obama atoa onyo kali kwa Urussi
Rais
wa Marekani Barrack Obama, ameonya Urussi kusitisha mpango wake wa
kutaka kutwaa eneo la Crimea nchini Ukraine lasivyo iwekewe
vikwazo.Akiongea katika Ikulu ya White House baada ya kufanya
mashauriano na kaimu Waziri Mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk, rais
Obama amesema nchi moja haiwezi kulazimisha taifa lingine kwa mtutu wa
bunduki.
Bwana Yatsenyuk amesema taifa lake sasa ni sehemu ya mataifa ya Magharibi na kamwe haliwezi kurudi nyuma.
Mabalozi katika Umoja wa Mataifa, wanasema Mataifa ya Magharibi
yanaandaa azimio la pamoja, katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
ambalo litakariri uhuru wa taifa la Ukraine na pia kuangazia kuhusu
kura ya maoni kuhusu itakayofanyika siku ya Jumapili, ikiwa eneo hilo la
Crimea litajitenga na kuwa sehemu ya Urussi.
Hata hivyo inatarajiwa kuwa Utawala wa Moscow utatumia kura yake ya
turufu katika baraza hilo la Umoja wa Mataifa kupinga azimio hilo.
No comments:
Post a Comment