Safari za treni katika eneo hilo zilisitishwa mara moja, huku pia vikosi vya usalama vikiliweka eneo hilo chini ya karantini huku takriban wafanyakazi 168 wa kwenye vituo vya nishati vilivyo katika maeneo ya jirani wakiwa wameondolewa katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, kampuni moja ya kutoa huduma za kusambaza gesi katika maeneo hayo, imeamuriwa kufunga huduma zake haraka iwezekanavyo, ili kuepusha majanga zaidi hii ikitokana na ukweli kuwa, kulisikika mlipuko mkubwa toka katika moja ya vyumba kwenye jengo hilo.
Raia mmoja ameeleza kuwa, amekuwa akisikia harufu ya gesi kila alipopita mahali hapo, kwa takriban wiki moja kabla ya tukio hili.
"Tuliona watu wakirushwa kutokea madirishani, hawa walikuwa majirani zangu, na kwa ujumla kishindo kilikuwa kikubwa sana kama bomu vile, na kilitetemesha jengo zima" ameeleza shuhuda mmoja, ambaye aliungwa mkono na shuhuda mwingine alyesema hali haikuwa tofauti na ilivyokuwa wakati wa tukio la kulipuliwa kwa majengo pacha kwenye sakata la September 11.
No comments:
Post a Comment