![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDaDmiNUVxO5F9EPMxHEilLzWKafUyj4EjbvOjt1ciTk9lNXZZ8lC7Iun170cdbiAQ3JQ_s_OigeLO-rAlsYvF7iRUBWOUq4_QrVwiTn5LZoTj-sL-07V0dFEmHzNXpwj8Pv68r0dzoq4/s1600/MalaysiaAirlinesBoeing777201.jpg)
Maswali yamebaki bila majibu kwa muda mrefu sasa lakini cha kushangaza
ni jinsi taarifa zinavyobadilika kila siku kuhusiana na nini kimetokea
kwa ndege hii.
Jambo la kwanza ilisemekana ndege imeangushwa na magaidi na tukaoneshwa
kuna abiria wawili wenye asili ya taifa la Iran ambao walipanda ile
ndege na pasi bandia. Bahati mbaya picha zilizotolewa zilionesha kitu
cha ajabu sana, abiria wale wawili picha zao ambazo zilipigwa dakika
chache kabla ya kupanda ndege zilionesha kufanana moja kwa moja tokea
kwenye kiwiliwili hadi chini. Wazo la Ugaidi likaanza kufa.
Jambo la pili, tumepewa sayansi kuwa ndege ilipotea ghafla kwenye Radar
za Malaysia ikimaanisha hapo ndipo ndege ilipoanguka. Kwa bahati nzuri
wote tunajua kila nchi ina jeshi na moja ya jukumu la jeshi ni kulinda
mipaka ya nchi, ardhini, majini na angani. Jeshi la Malaysia alikuwa
likizo, taarifa ni kwamba baada ya ndege kupotea kwenye radar za kiraia
za Malaysia iliendelea kuonenakana kwenye radar za jeshi kwa takribani
saa nzima ikionekana kubadili uelekeo na kuelekea magharibi hadi
ilipokaribia milango (Straits) ya Malacca ndipo ilipopotea kwenye radar
ya jeshi. Wakati ndege inapotea kwenye radar za kiraia ilikuwa inaruka
futi 36,000 lakini kwa mujibu wa radar ya jeshi, ikiwa Malacca ndege
ilikuwa umbali wa futi 29,500 kutoka usawa wa bahari. Kuna baadhi ya
wataalam wameeleza kuwa kutoonekana kwenye radar ya kiraia
kulisababishwa na kuzimwa kwa kifaa kinachofahamika kama Transponder
yaani kitambulisho cha ndege kwenye radar. Kwa wanaofahamu vizuri
masuala ya ndege watanielewa vyema, hiki kifaaa ni kitambuzi tuu na
hakiusiani na kuonekana ama kutoonekana kwenye radar na ndio maaana
kinapatikana kwenye baadhi tu ya ndege. Kuna maelfu ya ndege zinaruka
bila kuwa na hiki kifaa. Kwa sheria za anga ndege kubwa za abiria ni
lazima zifungwe transponder. Tukirejea kwenye radar, hii kazi yake ni
kutambua chochote kinachoruka kwenye anga la eneo husika iwe ni ndege,
puto au zile drones. Kutokana na hili, sababu iliyotolewa kuhusu
transponder ilipotoshwa mno tena na vyombo vingi vya habari vya
kimataifa na hata wachambuzi mbalimbali kwenye hili tukio. Ndio maana
radar za jeshi ziliweza kuendelea kuiona iyo ndege pamoja na madai ya
transponder kuwa off.
Jambo la tatu, kumekuwa na madai kuwa simu za mkononi za baadhi ya
abiria zilikuwa zikiita zilipopigwa siku kadhaa baada ya ripoti ya
kupotea kwa ndege. Hii inaashiria kuwa popote ilipo ndege kutakuwa ni
nchi kavu na eneo ambalo kuna maendeleo ya mwanadamu hoja kuu ikiwa
penye mawasiliano ya simu za mkononi lazima pawe na minara ya simu na
minara iyo kibiashara husimikwa kuzingatia na idadi ya watu
wanaopatikana katika eneo. Hili swala mpaka sasa halijakanushwa na
imeelezwa kuwa simu moja ilipokelewa na kukatwa. Kama ni kweli hiki ni
kiashiria kuwa ndege haijaanguka na ipo salama. Iwapo ingekuwa imeenguka
inamaana kufikia sasa ingeonekana kwa vile simu zimeita inamaana ipo
eneo lenye watu na hivyo mrejesho wa ajali ungepatikana.
Jambo la nne na ambalo halijapewa kipaumbele na media nyingin hasa TV,
ni kuwa katika ndege ile kulikuwa na abiria wasio wa kawaida, abiria
hawa wa kipekee ni wahandisi 20, 12 kutoka taifa la Malaysia na 8 kutoka
uchina. Hawa ni wataalam wa juu sana wa maswala yanayohusiana na
nishati mbadala pamoja na teknolojia inayohusu mambo ya kiusalama.
Wataalam hawa wanafanya kazi kule Austin, Texas kwenye kampuni inayoitwa
Freescale.
Utaona kwa hapo neno usalama (defense) alijitokezi lakini ni kwa sababu
mahususi, maswala ya usalama huwa hayawekwi wazi. Inawezekana kuna suala
la ugunduzi mpya wa teknolojia ya usalama na yenye maslai makubwa
walikuwanao. Kwa wenye kumbukumbu nzuri mwaka 1985 kuna wanataalam 17
wakijapan nao walikufa baada ya ndege yao kuanguka, jamaa hawa walikuwa
na ugunduzi wa mfumo mpya wa kuendesha kompyuta (OS) uliokuwa mahiri
zaidi ya ule wa Microsoft. Kawaida ugunduzi usajiliwa na muhusika kupata
hatimiliki inayoitwa PATENT, asilimia zaidi ya 90% ya patent usajiliwa
marekani au zinamilikiwa marekani. Ningeshauri wasomaji mfanye utafiti
zaidi hapa, kunawezakuwa na mengi kwenye hili jambo.
Jambo la tano, imethibitika kuwa pamoja na kuwa ndege ilipotea kwenye
radar zote za Malaysia baada ya kuvuka malango ya Malacca injini
zinaonekana kuendelea kufanya kazi kwa zaidi ya masaaa matano kwa mujibu
wa Boeing. Huu ni ushaidi kuwa ndege haikuanguka huko Malacca. Ndege za
boieng zimewekwa kifaa maalum cha kueleza ufanisi na ufanyaji kazi wa
injini za ndege, wakati ndege ikiwa angani kifaa hiki uendelea kurusha
taarifa kwa satelaiti ambayo uzichukua na kuzipeleka kwenye database ya
injini maintenance iliyopo makao makuu ya Boeing. Kwa bahati mbaya
satelaiti huwa hazina uwezo wa kueleza eneo (position) ya kituma taarifa
(transmitter) na hivyo ni ngumu kuweza kuto taarifa ya sehem ndege
ilipoelekea. Uhitaji zaidi ya satelaiti tatu kufanya kazi kwa
ushirikiano ili kuweza kutoa position ndivyo mfumo wa GPS unavyofanya
kazi. Hii imezidi kuhififisha hoja ya ajali yaani kuanguka. Hoja ya
ajali pia imeshindwa kwa kuwa nayo inazaa swali la iwaje black box
ishindwe kuleta signal na tunajua teknolojia ya black box sasa
imeboreshwa tangu ile ajali ya TWA Flight 800 na Air France Flight 447
zilizoangukia baharini.
Jambo la sita na jipya lililoanza alfajir ya leo ni kuwa ndege
inawezekana imetekwa na maharamia na imeelekezwa bahari ya hindi.
Bonyeza Missing plane: Piracy theory gains more credence. Ilianza dhana
ya magaidi wa ki-Irani na sasa tunaelekea kwenye uharamia wa bahari ya
hindi. Swali ni kama lengo la maharamia ni kuiangusha ndege kwanini
wasifanye hivyo kwenye Bahari ya kusini ya china na waelekee bahari ya
hindi? Tunajua kwenye meli wanaziteka zaidi zile za bahari ya hindi na
kuzipeleka karibu na Mogadishu sababu ndiko waliko na ngome kubwa na
nirahisi kuingiza na kutakatisha zile dola za ransom.
HITIMISHO:
Dalili zinaonesha kuna kuficha taarifa na kupindisha kwa makusudi
taarifa za hili tukio. Kutokana na kubadilika badilika kwa maelezo na
taarifa za msingi kutotolewa yawezekana kuna swala lenye maslai ju ya
ndege hii, abiria wake au mizigo iliyomo ndani. Ndege za karne hii
zimefungwa vifaa lukuki vya kurekodi taarifa, kuripoti taarifa, kutoa
onyo na hata kuiendesha ndege kiotomatiki pale parameter za rubani
zinapoonekana kuwa si sahii. Boeng 777 ni moja ya ndege zenye advanced
electronics system and Avionics, kwa hiyo lazima imeacha trace sehemu.
Dunia ya leo inateknolojia kubwa sana kuweza kutueleza yaliyojiri bila
taabu, si kama enzi za Titanic.
Kumeanza kuwa na wasiwasi wa ndege kuwa imeshambuliwa na kutekwa
kielektroniki na shirika lenye nguvu za kiteknolojia ambalo liliweza
kwanza kujam signal za ndege na hivyo kupelekea kuzimwa kwa transponder,
kufutika kwenye radar za kiraia na baadae za kijeshi. Teknoloji hii
hipo na mara nyingi imekuwa ikifanywa na yale madege yenye antenna kama
uyoga karibu na mkia, zinajulikana kama AWACS. Hizi uzipoteza signal za
radar za ardhini na kuficha ndege zilizo angani zisionekane na radar ya
aina yoyote. Majeshi ya marekani hutumia hizi sana kuzipoteza radar za
maadui wao wakati wa mashambulizi na kuzifanya zishindwe kuona ndege
zilizo angani. Mara nyingi huwa zinasindikiza fighter squadrons
zinapokwenda mstari wa mbele kwa kuzipa radar support na stealth cover.
Kwa hiyo kupatikana kwa ndege hii kunaweza zalisha mzozo mkubwa sana na
mlolongo wa maswali kutegemeana na wapi itakapopatikana, ikipatikana
ardhini maswali yatakuwa ni mengi mno maana nchi zote zilizo jirani na
ndani ya range ya uwezo wa ile ndege zina advanced radar kwa iyo
zingeiona tangu inaingia kwa anga yao.
Ikipatikana baharini nako ni maswali lukuki, maana bahari ya kusini ya
china inazaidi ya majeshi matatu highly advanced na kutokana na kuwa na
mzozo, yanafuatilia kinachoendelea angani na majini masaa 24. Yawezekana
ndio sababu ya hoja mpya ya leo asbui kuwa ndege itakuwa imetekwa na
maharamia na imepelekwa bahari ya hindi. Tunafaham huko hakuna uwepo wa
majeshi yenye kufanya monitoring ya maji na air space zaidi ya yale ya
marekani. Kwa wanaofahamu na waliobahatika kusafir na meli kutoka Asia
mpaka Africa watathibitisha hili jinsi walivyokutana na utitiri wa
monitoring ya wamarekani, ukitakiwa kuji-identify (kutoa taarifa za
chombo chako) kila baada ya masaa kadhaa.