Wakaazi wa mji mmoja kaskazini
mashariki mwa Nigeria wameonyesha hasira dhidi ya majeshi ya usalama kwa
kuondoa vituo vya ukaguzi kabla ya shambulio la wapiganaji wa Kiislam
katika shule shule moja katika eneo hilo.
Vijana wapatao 29 waliuawa katika shambulio
hilo, ambapo kikundi cha Boko Haram kimeshtumiwa kuishambulia shulehiyo
iliyopo jimbo la Yobe.Kituo kingine nje ya mji wa Buni Yadi pia walinzi wake waliondolewa wiki moja iliyopita.
Wanamgambo hao wa Kiislam waliishambulia shule hiyo usiku wa Jumatatu wiki hii.
Gavana wa jimbo la Yobe, Ibrahim Gaidam pia ameyashutumu majeshi ya usalama kwa ugoigoi mkubwa ulionyeshwa katika kukabiliana na tukio hilo, akisema saa tano zilipita bila ya askari wa usalama kuwasili katika eneo la tukio ili kuzima mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment