Monday, February 3, 2014

THAMANI YA MALI ALIZOKUWA ANAMILIKI HAYATI NELSON MANDELA ZATANGAZWA


Mandela alifariki mwezi Disemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 95
Hayati Nelson Mandela, aliachia familia yake mali yake yenye thamani ya dola milioni 4.1.
 Sehemu ya mali hiyo pia itatolewa kwa chama tawala ANC, wafanyakazi wake wa zamani na shule kadhaa ambako alisomea.

Hayo ndio yalikuwa mapenzi ya Mandela ambayo yalikuwa kwenye wasia wake uliosomwa hadharani kwa familia nzima.
 Afisaa Dikgang Moseneke aliyekabidhiwa jukumu la kusoma wasia huo wenye kurasa 40 na kuhakikisha unatekelezwa ,alisema hapajakuwa na pingamizi zozote kuhusu yaliyomo kutoka kwa familia ya Mandela.
 Wafanyakazi wa karibu wa Mandela watapata randi 50,000 kila mmoja. Shule ambazo Mandela alisomea zitapata randi laki moja kila shule.
 Hayati Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95.
 Familia ya Mandela tangu hapo imekuwa ikizozana kuhusu urithi wa hayati Mandela na kuna hofu kuwa huenda wasia huu ukasababisha mgogoro mwingine kuhusu mali hiyo.
 Mali ya hayati Mandela inajumuisha nyumba na hakimiliki za vitabu ikiwemo kimoja kuhusu maisha yake kwa jina ''Long walk to freedom'' 

No comments:

Post a Comment