IMEELEZWA
kuwa mkosaji na mvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ni serikali
kutokana na mazingira halisi ya utendaji na mfumo mzima wa utawala
katika serikali nyingi duniani.
Akizungumza
kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki
za Binadamu nchini, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)
kwa wakuu na makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, Jaji Mstaafu, Thomas
Mihayo amesema kwa mfumo wa utawala katika nchi nyingi duniani mkosaji
mkuu wa haki za binadamu ni serikali.
“dunia nzima
inajua kwamba serikali ndio mkosaji mkuu wa haki za binadamu na maana
halisi ya serikali ni dola na mahakama tu kwisha,” amesema Jaji Mihayo
Jaji Mihayo
amesema kuwa kwa hali ya kawaida dola ikimkamata mtu au mhalifu lazima
mpeleke katika mahakama ili sheria ichukue mkondo wake wa kawaida.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu,
Dkt Helen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi amesema warsha hiyo
inatoa fursa nzuri kwa watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi
kuboresha kazi zao za utetezi wa haki za binadamu nchini.Amesema kwa ujumla haki za binadamu hazipewi bali ni haki ya msingi ambayo mtu anazaliwa nayo ili zinaminywa aidha kupitia mtu kwa mtu au taasisi au mfumo wa utawala.
“Kazi za watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi zinaendama na msingi ni utetezi wa haki za binadamu pamoja na mali zao,” alisisitiza
Naye, Mratibu wa kitaifa wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake ya (The Concept of Protection and Security Management for Human Rights Defenders and Social Organization) amesema kuwa taaluma inaweza kutumika kutetea haki za binadamu katika maeneo mengi hapa duniani.
Amesema pia kupitia mada hiyo kwamba jamii inadhani kwamba anayepaswa kutetewa ni mwananchi tu lakini pia hata polisi naye ni binadamu anapaswa kuwa na mtetezi pale ambapo haki yake ya msingi inapovunjwa.
“Mpaka sasa Tanzania haina sheria yeyote inayomlinda mtetezi wa haki za binadamu lakini tunaendelea na mchakato na ni matumaini yetu serikali itaridhia kuwa na sheria hiyo hapa nyumbani,” alilisitiza
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki amesema kuwa jeshi la polisi nchini litaendelea kuimarisha mahusiano kati ya jeshi hilo na watetezi wa haki za binadamu nia ni kudumisha amani na utulivu nchini.
“majukumu ya jeshi la polisi na watetezi wa haki za binadamu nchini yanafanana kwa kila hali ni kulinda na kutetea haki za wananchi na mali zao,” amesema Naibu IGP Kaniki
Kamishina Kaniki alilisitiza kwamba ni muhimu wadau wote kuzingatia sheria za nchi, taratibu na kanuni katika kutafuta haki mbalimbali ili kudumisha amani na utulivu nchini.
“nachukua nafasi kuwakaribisha wadau wote wa haki za binadamu na makundi mengine kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda na kutetea haki za binadamu nchini,” alisisitiza.
Kamanda wa Polisi Arusha, RPC Liberatus Sabas amesema kwa muda mrefu watu wa utetezi wa haki za binadamu na makundi mengine huwa wanasahau kwamba polisi pia ni binadamu nao wanahitaji utetezi kutoka kwa watetezi hao wa haki za binadamu.
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdurahman Kaniki, akitoa hotuba yake
ya ufunguzi kwa niaba ya IGP Ernest Mangu, kwenye warsha ya siku moja
iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki
za Binadamu nchini.
Mjumbe wa
Bodi ya Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (Tanzania Human
Rights Defenders Coalition) Dk. Hellen Kijo Bisimba akitoa neno la
ufunguzi wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha watetezi wa Haki
za Binadamu nchini na Jeshi la Polisi jijini Dar.
Jaji
Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi
nchini, umuhimu wa kushirikiana kati ya Jeshi hilo na Asasi za kutetea
Haki za Binadamu ili kuleta tija katika nyanja za kiuchumi, kijamii na
kisiasa.
Sehemu ya
makamishina na makamanda wa mikoa na maafisa waandamizi wa Jeshi la
Polisi nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku
moja jijini Dar es Salaam.
Naibu
Inspekta General wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki (kushoto),
Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa (katikati) pamoja na
Mkurugenzi wa Mafunzo na Oparesheni, Kamishina Paul Chagonja
wakifuatilia mbalimbali ilizokuwa ikitolewa na washiriki wa warsha hiyo.
Mratibu wa
THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake juu ya Ulinzi na
utawala wa haki za binadamu kwa mashirika ya watetezi wa Haki za
Binadamu pamoja na Polisi.
Pichani
juu ni Meza kuu na chini ni Baadhi ya Wakuu na Makamishina wa Jeshi la
Polisi nchini wakifurahia jambo wakati wa uwasilishwaji wa mada
mbalimbali kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi
waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Kamishina
wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova akichangia mada
katika warsha ya siku moja kuhusu Haki za Binadamu na ushirikiano kati
ya Jeshi la Polisi na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Kamanda wa
Polisi, Arusha Liberatus Sabas akizungumza umuhimu wa kujali pia askari
polisi kwa sababu na wao pia ni Binadamu wanahitaji utetezi kutoka kwa
mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea Haki za Binadamu nchini.
Kamanda wa
Polisi, Lindi, RPC Zeloithe Stephen akitoa nasaha kuhusu miiko na kanuni
za Jeshi la Polisi jinsi zinavyotetea na kulinda Haki za Binadamu
(Police General Order).
Picha ya pamoja kati ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini na mgeni rasmi Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Malya (kulia) akiteta jambo na Kamishina wa
kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova baada ya kupiga picha
ya pamoja.
No comments:
Post a Comment