Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi
wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati
alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar
es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah
Chuoni February 27, 2014. Nyuma yake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha
Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe saidi Meck Sadick.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waombolezaji wengine kwenye hafla rasmi
ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi
Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni February 27, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akifariji familia ya marehemu kwenye hafla rasmi
ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi
Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni February 27, 2014.
PICHA NA IKULU
Rais Kikwete aliwasili kwenye ukumbi huo kujiunga na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waliokuwa Mawaziri Wakuu, Joseph Warioba na Frederick Sumaye, Makamu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Rwekaza Mukandala, familia ya marehemu na waombolezaji wengine muda mchache klabla ya kuanza shughuli ya kuaga mwili.
Marehemu Kazaura ambaye alikuwa Mkuu wa UDSM kati ya mwaka 2005 hadi kifo chake, aliaga dunia Jumamosi iliyopita katika Kituo cha Ugonjwa wa Kansa mjini Chennai, India na mwili wake uliwasili nchini Jumanne wiki hii. Mazishi ya marehemu yamepangwa kufanyika keshokutwa Jumamosi, Machi Mosi, 2014, nyumbani kwao Bukoba.
Katika uhai wake alishikilia nafasi nyingi za utumishi ikiwa ni pamoja na kuwa RDD, Katibu Mkuu wa Wizara mbali mbali, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya na Ubelgiji, na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment