Sunday, February 2, 2014

SIRI 7 ZA KUVUNJA NDOA NA MBUNGE MZEE!


YULE ‘hendsam’boi’ Michael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) na miezi michache mbele ndoa ikavunjika, ameibuka na kuanika siri 7 zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar, juzi,…
Stori: Imelda Mtema na Ojuku Abraham YULE ‘hendsam’boi’ Michael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) na miezi michache mbele ndoa ikavunjika, ameibuka na kuanika siri 7 zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar, juzi, Michael alibainisha mambo hayo huku akisema anajuta kwa tukio lile ambalo bado halijamtoka kichwani hadi sasa.
Michael Christian‘hendsam’boi’, alipotua ndani ya  Ofisi za Global jijini Dar.
SIRI YA KWANZA
Kijana Michael aliianika siri ya kwanza kwamba ni kuchekwa na marafiki zake wa Bagamoyo mara baada ya kugundua amefunga ndoa na mbunge huyo ‘mzee’.
“Marafiki zangu walianza kunicheka, walisema nimefunga ndoa na mbunge mzee, mama mtu mzima. Nikaanza kujisikia vibaya jambo ambalo sikulipenda hata kidogo,” alisema kijana huyo ambaye ni yatima.

SIRI YA PILI
Akizungumza kwa hisia kali, Michael aliye na taaluma ya uuguzi, aliiweka wazi siri ya pili ya kuamua kuivunja ndoa yake na mheshimiwa huyo kuwa ni kitendo cha kutokuwepo kwa tangazo la ndoa la siku 21 kama sheria ya nchi inavyotaka.
Kuna kifungu cha sheria kinachotaka wachumba wanapotaka kufunga ndoa kutolewa tangazo la siku 21 kwenye mamlaka za kufungisha ndoa hiyo ili kama mmoja wa wahusika ana ndoa inayoishi (halali) aweze kuwekewa pingamizi la kufungishwa ndoa.
SIRI YA TATU
Kijana huyo aliendelea kwa kuifunua siri ya tatu kuwa ni kitendo cha kufungishwa ndoa bila kuwepo na mashahidi wa pande zote mbili (matroni na patroni) walioandaliwa zaidi ya kuitwa papohapo.
Alimtaja kwa jina moja Mchungaji Mtetumo wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’ kuwa ndiye aliyesimamia kufungwa kwa ndoa hiyo, Septemba Mosi, 2011 ndani ya ofisi huku milango ikiwa imefungwa.
Alisema pia kwamba, suala la ndoa aliligundua siku hiyohiyo baada ya kufika kwenye kanisa hilo ambapo maandalizi mengine yote yalishafanyika akiwa hajui.

SIRI YA NNE
Siri zilizidi kubanjuliwa, Michael alisema sababu ya nne ambayo pia ilimsukuma kuamua kubatilisha ndoa yake na mama Kasikila ni baada ya kubaini kwamba, hataweza kupata uzao kwa mke huyo kwa sababu ana watoto wakubwa kiumri kuliko yeye.
“Nilijua sitapata watoto, hakukubali kuzaa na mimi kwa sababu tayari ana watoto wakubwa, mimi mdogo, ingekuwa vigumu. Kifupi haikuwa ndoa halali kwangu,” alisema kijana huyo.

SIRI YA TANO
Michael: “Alianza kunibana sana, kila hatua ya miguu yangu alitaka kujua inakwenda mpaka wapi! Hii hali nikaiona inanipiga pingu, nikagundua kuwa kumbe mimi sijaoa, bali nimeolewa. Yule mama alinioa mimi, si kwamba mimi nilimuoa yeye, nikasema ili niwe na amani ya moyo ni lazima ndoa ivunjike.”

SIRI YA SITA
Kijana huyo hakuona sababu ya kubakiza siri hata moja, akaendelea kuzianika:
“Jambo jingine ambalo pia lilichangia kuamua kuivunja ndoa ile ni baada ya kukumbuka historia ya kukutana kwetu.
“Wakati nipo Hospitali ya Bagamoyo na yeye akiwa pale kama muuguzi mkuu, tulizoeana. Kuna siku aliniita kwake akasema anasafiri anaomba nimwangalizie nyumba, nilikuwa na rafiki yangu tukawa tunalala pale mpaka aliporudi.
“Kuzoeana kuliendelea, mwishowe tukawa wapenzi mpaka ndoa. Nilipokumbuka hivyo tu nikagundua kuwa aliniingiza mapenzini kwa hila au mbinu, hilo pia sikulipenda,” alisema Michael.   

SIRI YA SABA
Michael alisema sababu ya saba ambayo pia ilimshinikiza kuivunja ndoa hiyo ni kupwaya ndani ya nyumba.
Alisema kutokana na umri wake, ndani ya nyumba alijiona ni mtoto na si mume kama wanaume wengine walivyo.
“Hata uwezo wangu wa mawazo kwake haukuwa wa mume na mke, ni wa mtoto na mama. Kifupi haikuwa ndoa halali,” alisema.

SIKU ALIPOIVUNJA NDOA
Kijana huyo alisema ndoa yake na mheshimiwa huyo aliivunja mbele ya Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God, Dk. Getrude Rwakatare walipokwenda kusuluhishwa ili waende wakaishi kwa amani.
Alisema kabla ya usuluhishi alimfungukia mama Rwakatare kuhusu manyanyaso anayoyapata ndani ya ndoa hiyo ndipo aliposimama na kuivua pete kisha kuitupa chini huku akisema katu hawezi kurudi kwa mkewe huyo na ndoa imevunjika, akaondoka zake.

ANATAKA KILIO CHAKE KIFIKE KWA JK
Kijana Michael alisema kilio chake kikubwa kwa sasa ambacho angependa kifike hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ni kitendo cha mkewe huyo kuzuia vyeti vyake ambavyo vingemsaidia kutafutia kazi sehemu mbalimbali.

“Amezuia vyeti vyangu vyote, kila nikimwambia navitaka nikienda ananifanyia visa, nawaomba Watanzania wanisaidie kwa hili.
“Mimi kwa sasa nataka vyeti tu, sitaki cha ndoa wala nini? Lakini hataki kunipa,” alisema Michael.

MSIKIE MBUNGE SASA
Akijibu tuhuma hizo, Mheshimiwa Kasikila alikiri kuwa na vyeti vinavyolalamikiwa na mumewe huyo, lakini alikanusha kwa nguvu zote juu ya maneno kuwa yeye ameoana na mtoto mdogo, akirejea vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinavyomtaja mtoto kama ni mtu wa namna gani.
Mbunge: “Mwandishi, unafahamu mtoto kwa katiba yetu ni mtu wa namna gani?”
Mwandishi: “Ni mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane.”
Mbunge: “Sasa Michael ni mtoto? Ana miaka 28 unamuita mtoto?”

AWAWEWESEKEA WANASIASA
Alisema anajua suala hilo lina shinikizo la kisiasa, kwani hivi karibuni baadhi ya wanasiasa walikwenda jimboni kwake wakiwa na nakala ya gazeti moja lililoandika habari zake na kijana huyo na kuwaambia wapigakura wake kuwa mbunge wao ameoa kitoto, lakini wapigakura wake waliwapuuza kwa kuwaambia hilo haliwahusu kwani wanachojua anawawakilisha vizuri bungeni.
“Kama kweli ninyi mnampenda huyo Michael, muelekezeni sehemu sahihi ya kwenda kupeleka madai yake. Ngoja nikupe mfano, mimi nikiwa wizara ya afya, mtu akija na malalamiko kuhusu pembejeo za kilimo, kwa kumsaidia, nitamuelekeza aende wizara ya kilimo, kwa kuwa pale (afya) siyo sehemu yake, sasa nyinyi muelekezeni huyo sehemu sahihi ya kupata haki yake, siyo huko magazetini,” alisema mama huyo.

No comments:

Post a Comment