Umoja wa mataifa unakadiria
kwamba takriban watu millioni 3.7 nchini Sudan kusini wanakabiliwa na
uhaba wa chakula kutokana na mapigano kati ya vikosi vya serikali na
waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.
Mratibu wa maswala ya kibinaadamu katika umoja
huo Toby Lanzer ameiambia BBC kwamba mzozo huo ulioanza mwezi Disemba
mwaka jana umeharibu masoko pamoja na maisha ya kawaida ya watu, mbali
na kusababisha hali mbaya ya kibinaadamu kwa thuluthi moja ya idadi ya
raia.Na ili kuzuia Janga ,amesema kuwa umoja wa mataifa unahitaji dola millioni 1.3 pamoja na mazingira yalio salama ili kutekeleza wajibu wake.
Maelfu ya raia wamepoteza maisha yao katika vita hivyo ambavyo umoja wa mataifa unasema vinaendelea licha ya kutiwa saini kwa mkaaba wa kuvisitisha ju
No comments:
Post a Comment