Tuesday, February 25, 2014

Shambulio dhidi ya Al Shabaab

 
Kikosi cha Umoja wa Afrika kimeongezeka idadi na kufika 22,000
Wanajeshi wa Ethiopia, wengi wao ambao tayari wapo Somalia, wamejiunga na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika, na sasa kina uwezo wa wanajeshi 22,000.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la mashambulio ya Alshabaab katika wiki za hivi karibuni hususan katika mji mkuu Mogadishu.
Waziri mkuu wa Somalia, Abdiweli Sheikh Ahmed siku ya Jumatatu alisema, serikali haitoliruhusu Al shabaab, 'kujificha na kutushambulia tena.'
Al Shabaab 'Haiogopi'
Mwandishi wa BBC amezungumza na mfuasi wa Al shabaab aliyepuuzilia mbali uwezekano wa shambulio hilo dhidi yao.
Alisema, "Hatuna wasi wasi, hakuna ishara yoyote ya shambulio hilo. Na hatahivyo tumekuwa tukipigana tangu 2007 na ni vizuri mtu kufariki kwa ajili ya dini yake."
Kwa uwezakano wowote ule, wa kutokea shambulio hilo, Al Shabaab litaidhinisha mbinu yake inayoitaja kuwa 'mbinu ya kujiondoa', kutoka katika miji linayoyadhibiti.
Katika kukabiliana na kikosi chenye nguvu zaidi, Al shabaab haipendelei kupoteza wafuasi wake na rasilmali zake kwa kuzipigania.
Mwandishi wa BBC aliliuliza kundi hilo kuhusu ongezeko la ghasia katika mji mkuu Mogadishu pamoja na milipuko ya kujitoa muhanga, mashambulio ya grinedi na mauaji ya kulengwa.
Kumekuwa na ongezeko la mashambulio hivi karibuni
Ongezeko La Mashambulio
Kwa sasa kundi hilo pia linatekeleza mashambulio ya makombora usiku katika wilaya kadhaa kwa wakati mmoja, na kupigana mchana na vikosi vya Umoja wa Afrika na jeshi la Somalia.
Mfuasi huyo wa Al Shabaab alisema hayo yote hayahusiani na uwezekano wa shambulio hilo dhidi yao, bali ni njia yao ya kuwaonyesha watu kwamba Al Shabaab lingalipo mjini.
Ukumbusho mkali ni shambulio la hivi maajuzi katika ikulu ya rais, wakati kundi hilo lilipigana na kupita baadhi ya vizuizi vya ndani ya eneo la ikulu hiyo.
Hili ni eneo linalopaswa kuwa na ulinzi wa hali ya juu katika nchi nzima a Somalia.
Iwapo serikali,kikosi cha Umoja wa Afrika, washauri wa kutoka mataifa ya magharibi na wengine wa usalama hawawezi kuilinda ikulu, kuna matumaini kidogo kwamba wataweza kuilinda sio tu nchi nzima, bali eneo lililosalia la Mogadishu.

No comments:

Post a Comment