Robina, mwenyeji wa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara ambaye alikuwa anasoma katika shule ya wasichana ya Marian, akiwa na ndoto ya kuwa daktari wa watoto amejibu maswali kumi muhimu na majibu yake yanaweza kuchukuliwa kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi walioko shuleni ambao wanakumbwa na changamoto kadhaa, na wazazi wanaowapeleka watoto wao shule.
Ulifanya nini ghafla ulipopata taarifa kuwa umekuwa wa kwanza Tanzania nzima, na je, ulitegemea?
Nilipopata matokeo kwamba nimekuwa wa kwanza, kwanza nilifurahi sana na kilichobaki zaidi ilikuwa ni kumshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiye kayawezesha yote. Nilihisi kama kupaa vile…nilifurahi sana halafu my mom alikuwa pale… alikuwa analia akaniinfluence na mimi machozi yatoke, I was very happy yaani. Sikutegemea kuwa wa kwanza lakini nilikua na uhakika wa kufanya vizuri kwa sababu niliplan kufanya vizuri.
Kama msichana ulifanya nini kuzivuka changamoto za kimasomo na kufanikisha kwa kiasi kikubwa?
Safari ya taaluma ni ndefu ndio, kwenye safari ya masomo kuna changamoto za hapa na pale, ambapo mara nyingi wasichana waga tunafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Lakini kwangu mimi nimeweka interest yangu sana kwa wazazi. Kwa hiyo nilikuwa open kwa wazazi na kuwaomba ushauri wa hapa na pale nifanye nini. Na katika vyote nilivyokuwa nafanya ni kufanya kile kitu ambacho hakiwezi kusubiria kwanza ambacho ni masomo. Kwa hiyo naweka juhudi pale ili ukishafanya kila mtu ajue kwamba umefanya.
Ilikuwa mbaya sana kwenye kusoma hasa form three ambapo nilianza kushuka and all that. Kwa hiyo wazazi pamoja na walimu pia walikaa na kuweza kunisaidia na mimi mwenyewe nilikuwa tayari kusikia ushauri wao na kuweza kusoma kwa bidii zaidi ili niweze kupata ile nafasi yangu niliyokuwa naipata toka nianze.
Nini kilichofanya ushuke kimasomo wakati huo?
Kilichofanya nishuke ni ile kupoteza malengo na juhudi zangu, na pia kuona kwamba vitu vinaanza kuwa vigumu halafu kuweka hiyo kwenye akili kwamba hicho ni kigumu siwezi kukifanya. Lakini nilipoamua kuweka juhudi na kuona kwamba ni vitu vya kawaida kwamba navyozidi kukua na vitu vinazidi kuwa vigumu na natakiwa nitafute njia ya kuvi-overcome, ndo hivyo nikaweza kufanikiwa.
Ratiba yako ya siku ulipokuwa shule kwa ujumla wake ilikuwa vipi na muda gani ulikuwa unajisomea?
Asubuhi nilikuwa naamka mapema kabla ya time table ya shule haijaanza kwa sababu tunatakiwa tuamke mapema kwenda misa kwenye saa kumi na moja hivi. Kwa hiyo naamkaga kwenye saa tisa najiandaa naenda darasani kwa sababu siwezi kusoma usiku kwa sababu usiku nakuwa nimechoka, kwa hiyo my extra time inakuwa asubuhi ambako I’m still fresh.
Nasoma then ikifika muda wa misa naenda kusali. Nikitoka kusali kuna kazi ndogo ndogo za kufanya kujiandaa na time table ya school and all that. And my free time ile mchana nikitoka darasani kuanzia saa nane, nakuwa nimepanga nini natakiwa nifanye, ni somo gani natakiwa kulisoma at that time ambapo ni saa nane mpaka saa kumi na nusu. Ambapo ni muda wa concentration, kama kuna kitu ambacho sijaelewa naenda kuwafuata waalimu kwa sababu wanakuwa wapo at that time. And kuna some free time kama ile break time, ni kuanzia saa nne na dakika 40 mpaka saa tano na robo, pale hauwezi kusema unatake breakfast all the time, unatake breakfast for a short time halafu nyingine inabaki unaweza kufanya maswali matano ya physics. Yaani every little time ambayo unaweza kuipata, you don’t let it go to waste tu, una-utilize.
Marafiki ulionao wanaweza kusaidia kukupandisha au kukushusha. Wewe ulikuwa na marafiki wa aina gani?
Marafiki wangu nimewachagua kwa category..yeah (anacheka), ikifika muda wa kusoma nakuwa na mtu ambaye najua atanisaidia, kwa hiyo nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Sarafina amekuwa wa nne. Alikuwa ananiinfluence sana kusoma, huyo ni wakati wa kusoma, kwenye academics namfata yeye.
Ikifika wakati wa social siwezi kumfata sarafina kwa sababu she is not that social, yeye yuko kama mimi we are not that social, kwa hiyo ninaye social friend. Pia ikifika muda wa kuspend, I have an economical friend. Ambaye I’m sure nikikaa nae nikiwa naspend siwezi kwenda beyond my budget. Kwamba siwezi kufulia. Kwamba we are all in the same status, same friends, yeah.
Ni kitu gani kilikuwa kinakuboa sana shuleni na kukunyima furaha muda mwingine?
Kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana, ikifika wakati ambapo kwa mfano watu wachache kwenye darasa wamefanya kosa halafu sasa mnakuwa included as a whole class halafu mnapata adhabu. Hiyo adhabu directly itaharibu time table yangu ya kusoma. Kwa hiyo badala ya kusoma nafikiria ningekuwa nasoma physics, I’m either slashing an area..yaani hiyo ilikuwa inaniboa sana yaani.
Ulishawahi kuitwa ‘Msongo’ au majina kama hayo? Ulikuwa unaichukuliaje na je, ilikutenga na marafiki zako?
Yeah, msongo…kauzu. Yeah mimi naipenda hivyo kwa sababu nafanya nachotakiwa kufanya ambacho ni kusoma. Hiyo haikunitenganisha na marafiki zangu.
Vuta taswira, je, ingetokea ukapata division Zero na kuwa wa mwisho Tanzania nzima ungefanyaje? Na unawashauri nini waliofeli kwa kiasi hicho?
Kama ningepata zero, kwanza ningefikiria…na ningekuwa very disappointed kweli, lakini pia ningefikiria kuhusu kujipa second chance, ningeenda kusoma tena.
Kwa waliofeli ningependa kuwashauri wasikate tamaa hata kidogo and wajipe second chance. Kwa wengine pia ambao wana vipaji vyao wanaweza kuviendeleza. But pia kwa kuwa elimu ni muhimu..ku-reseat pia ingekuwa ana option.
Robina Nicholaus ni msichana wa aina gani?
Robina ni mtu mkimya lakini mcheshi pia. Nisingependa nikae na mtu halafu nikawa kimya just because ni mkimya... I will try kuchekesha, and of course I’m funny anyway.