Tuesday, April 16, 2013

RPC MKOANI KAGERA AWAONYA WAARIFU WANAO JIFICHA KWENYE UENDESHAJI WA PIKIPIKI

 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Alex Kalangi amesema baadhi ya makundi ya wahalifu yanajificha kwenye shughuli za uendeshaji na usafirishaji wa abiria maarufu mjini Bukoba kwa jina la Asecdo.
Akitoa ufafanuzi wa zoezi lililofanyika mwishomni mwa wiki la kukamata vyombo vya usafiri hasa pikipiki,Kamanda Kalangi amesema zoezi hilo ni endelevu ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kuwatia mbaroni wahalifu sugu.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliohoji uhalali wa Polsi kutumia nguvu kubwa dhidi ya waendesha pikipiki wasio na silaha,Kamanda Kalangi amesema waendesha pikipiki hao baadhi walikaidi amri ya Polisi na hata kujipanga kukabiliana nao.
Hata hivyo alisema waendesha pikipiki wengi wanaendesha shughuli zao kwa kufuata sheria na kuwaonya baadhi yao wanaotumiwa na makundi ya wahalifu kuwa Polisi hawatasita kuwachulia hatua kali.
Pia Kamanda Alex Kalangi amewaomba waendesha pikipiki wa mjini Bukoba kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa za kuwabaini wahalifu wanaojificha miongoni mwao ambao wanatia doa ajira yao ya usafirishaji wa abiria.
Kwa mujibu wa Kamanda Alex Kalangi katika zoezi hilo zaidi ya pikipiki thelathini zlikamatwa,na kuwa uchunguzi wa kuwabaini waendesha pikipiki waliokuwa wamejiandaa kuwashambulia askali Polisi unaendelea.
 Kamanda Alex kalangi akionyesha sehemu ya pikipiki zilizokamatwa wakati wa zoezi hilo na kuhifadhiwa kituo cha Polisi mjini Bukoba
 Baadhi ya maaskali wa pikipiki wanaohusika na zeezi hilo,wajiandaa kuingia kazini

No comments:

Post a Comment