Tuesday, April 9, 2013

RAIS KIKWETE AWASILI NAIROBI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS WA NNE WA KENYA MHE UHURU KENYATTA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi jana tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nne wa Kenya, Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake, Mhe. William Ruto, katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo Aprili 9, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni  baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nne wa Kenya, Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe. William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo Aprili 9, 2013. Mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batilda Burian wamesimama pembeni na wenyeji wao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nne wa Kenya, Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe. William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo Aprili 9, 2013.
(PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment