Wednesday, April 17, 2013



Kila ndoto naamini ina maana ila kwa bahati mbaya
Sio kila mtu ana uwezo wa kufahamu nini maana ya ndoto.
Naamini kila mtu huwa anaota
Ndoto zingine unazikumbuka ukiamka na nyingine huzikumbuki kabisaaa

Katika ndoto tunazoota huwa kuna
Mazuri, mabaya, dilema au hata vya kutisha.
 Nilipolala usiku wa kuamkia Jumatatu niliota ndoto tatu, mbili nilizikumbuka na moja niliisahau.

Naomba kusimulia ndoto zangu.

NDOTO 1:

Niliota nimejikuta mbele ya Nyumba ya mama wa mtu ninaemfahamu, Nyumba hiyo ilikuwa na kamba za kuanikia nguo, na nguo zikiwa zimeanikwa, mbele ya nyumba ya mama huyo pia kulikuwa na ndoo zimezagaa mbele ya nyumba na nyumba ilikuwa haijaisha kujengwa. (Pagale)
Mama wa mtu niliemuota sijazoeana nae zaidi ya salaaam.

Lakini mbele ya nyumba ya mama huyo nilikuwa nikiomba hifadhi usiku wa manane, bila kujua nilifikaje, wakati niko ndani  ya gari ndogo mfano wa Starlet.
Ambayo ilikuwa ni ndogo kuliko hata ndoo ya maji lakini sijui niliweza vipi kutosha ndani ya gari hiyo, niliendelea kupiga honi lakini hakuna alietoka wala sikuona mtu pembeni.

Zaidi ya mbwa wakubwa, weusi watatu, wakubwa kuliko hiyo gari.
Wakaanza kufoka na kushambulia gari kwa kung'ata matairi na kung'ata vioo
Walikuwa na nguvu kuliko mbwa wa kawaida niliopata kuwaona hapa duniani.

Mwisho mpaka nazinduka ni kwamba.
Sikung'atwa na wale mbwa, yule mama niliekuwa nampigia honi hakutoka kwenye ile nyumba
Na wala sikuona hata jirani yoyote kutoka labda kusema mwizi, mwizi
Na ndoto ikaisha nikazinduka, kama ilivyo kawaida ya ndoto hazifikagi mwisho.

NDOTO NO 2:

Kulikuwa na Gardner wawili, mmoja mrefu size ya Gardner wangu wa kawaida ninaeishi nae.
Mwingine mfupi na ana alama nyeusi kama mtu aliewekwa alama kutumia moto usoni.
Yule Gardner mfupi akaanza kugombana na mimi kwa kunishambulia kiasi cha mimi kushindwa kujitetea, alinishambulia sana kwa muda mrefu.
Gardner mrefu alipotokea akauchukua ule ugomvi wakaendelea kupambana
Sikujua ugomvi ulivyoendelea lakini ndoto ikaishia hapo.

NDOTO NO 3:
Bahati mbaya hii sikuikumbuka.

OMBI:
Ila napenda kufahamu kuna yeyote anaelewa maana ya ndoto hizi?? Na je! yupo pia anaeelewa maana ya kusahau ndoto.
Na unaipataje ndoto ulioiota ukaisahau, unaikumbukaje yani?

No comments:

Post a Comment