Thursday, October 24, 2013

YANGA YAUA TAIFA, SIMBA YASHIKWA SHARUBU TANGA


Wachezaji wa Simba SC, Haruna Shamte (kushoto) na Joseph Owino wakijadiliana jambo baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Coastal Union leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga. (Picha na Richard Bukos / GPL,TANGA).

Yanga SC leo imeweka kimbindoni pointi tatu baada ya kuichabanga mabao 3 - 0 timu ya Rhino Rangers kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Hamis Kiiza aliyefunga mawili katika dakika ya 12 na 81 wakati lingine likifungwa na Frank Domayo mnamo dakika ya 72.


Wakati Yanga wakitoka vifua mbele leo, watani wao Simba SC wao wameshikwa sharubu baada ya kulazimishwa sare ya 0 - 0 na Coastal Union ya mkoani Tanga. Mechi hiyo imepigwa katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment