Polisi wa Misri wamefyatua
moshi wa kutoza machozi kuvunja maandamano mjini Cairo, ya wanafunzi
wanaomuunga mkono rais wa zamani, Mohamed Morsi.
Mawe yalirushwa na pande zote mbili huku
wanafunzi mia kadha wakijaribu kutoka chuoni kuelekea Medani ya Rabaa,
pahala pa kambi ya wafuasi wa Morsi ambayo ilifungwa na wakuu miezi
miwili iliyopita.Hii ni siku ya pili ya mapambano katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambako kuna wafuasi wengi wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bwana Morsi.
Bwana Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwezi wa Julai.
No comments:
Post a Comment