Monday, October 21, 2013
HATIMAYE JICHO PEVU WATOA VIDEO YA MAKALA INAYOELEZEA UKWELI WA TUKIO LA WESTAGATE ANGALIA HAPA
Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa,
zimekuwa siku nyingi za kubashiri, na siku nyingi za kunongonezana
kuhusu kilichojiri wakati taifa lilitekwa nyara na magaidi kwa siku nne
mtawalia. Wakenya zaidi ya sitini walipoteza maisha yao katika jumba la
Westgate lakini hadi sasa Wakenya hawajajua ukweli kuhusu yaliyojiri
katika jumba la Westgate. Je ni kweli kuna waliokuwa wametekwa nyara na
magaidi na kuzuiliwa katika jumba hilo? Je ni kweli kuna magaidi
waliouawa na wanajeshi? Meza ya upekuzi ya Jicho Pevu na Inside Story
usiku na mchana wamekuwa wakidurusu kila ukurasa na, kufanya mahojiano
na kupitia hatua kwa hatua video za cctv kutoka jumba la Westgate na
sasa wako tayari kukusimulia kilichojiri bila kuficha lolote. Meza hii
ilifanikiwa picha za pekee kuhusu matukio ya Westgate. Usiambiwe tena
tizama makala haya yatakayokujia katika muda usiokuwa mrefu ukiwanaye
mwanahabari mpekuzi mohammed ali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment