Sunday, April 14, 2013

JOHARI AGOMA KUKATA MAUNO

MKONGWE kwenye ‘Industry’ ya Filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alitoa kali ya aina yake baada ya kukataa kuzungusha nyonga mbele ya mwigizaji mwenzake, Vincent Kigos ‘Ray’ anayedaiwa ni mpenzi wake.
Tukio hilo lililonaswa na paparazi wetu juzikati, lilitokea katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wakati wasanii hao walipojumuika pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kitokee kifo cha msanii mwenzao, Steven Kanumba.
Akiwa viwanjani hapo, Johari aliitwa kupanda jukwaani na wasanii wenzake kwa ajili ya kucheza sebene kidogo lakini yeye alikataa na paparazi wetu alimsikia akijitetea kuwa hawezi kukata nyonga mbele ya wasanii wenzake hususan Ray ambaye ni bosi mwenzake kwenye kampuni yao ya RJ Company.
“Siwezi kujidhalilisha mbele ya umati huo kwa kukata kiuno tena na bosi mwenzangu yupo pale, labda ningekuwa nimelewa kiasi cha kutojitambua hapo ningefanya madudu kama hayo,” alisema Johari.

No comments:

Post a Comment