Monday, April 29, 2013

ANAETAJWA KUWA MRITHI WA JOSE MOURINHO


Kocha wa Paris St Germain Muitaliano Carlo Ancelotti ametajwa kuwa mbioni kurithi nafasi itakayoachwa wazi na Jose Mourinho kama kocha wa Real Madrid ambapo inasemekana Ancelotti tayari ameingia kwenye makubaliano yasiyo rasmi na atachukua nafasi hiyo siku chache baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Moja ya tetesi ambazo zimejaza kurasa za magazeti yenye habari za michezo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni ile inayohusu Jose Mourinho kuondoka kwenye klabu ya Real Madrid ambako amekuwa hana mahusiano mazuri na baadhi ya watu akiwemo nahodha Iker Cassilas na baadhi ya viongozi.

Carlo Ancelotti kwa upande wake amekuwa akihusishwa na taarifa za kufukuzwa kazi na mabosi wa Paris St Germain ambao wamekuwa hawafurahishwi na aina ya soka linalochezwa na klabu hiyo pamoja na usajili mkubwa ambao imeufanya, uongozi wa Real Madrid unaamini kuwa Ancelotti ana uzoefu na uwezo wa kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ulaya kama alivyowahi kufanya mara mbili akiwa na Ac Milan pamoja na Juventus ambayo aliiongoza kufika fainali ya michuano hiyo.
Kama Real Madrid itatolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa ambako iko nyuma kwa mabao manne baada ya mchezo wa kwanza, mwisho wa Jose Mourinho utakuwa umekaribia kwani atakuwa ameshindwa kuipa klabu hiyo mafanikio iliyotarajia ya ubingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 11.

No comments:

Post a Comment