Wednesday, April 17, 2013

BAADA YA UWOYA KUNASWA HOTEL NA DIAMOND NDIKUMANA AZIMIA

HAYA SASA!
Mapenzi bwana! Ukiambiwa yanaweza kuua usibishe kabisa, kwani ukiondoa mifano mingine ya kufikirika, kitu ‘live’ ni kwamba mwanasoka raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alianguka na kuzimia, baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu mkewe.

Ndikumana, alianguka na kuzimia, asubuhi ya Aprili 8, mwaka huu, baada ya kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda, lililoandika habari ya usaliti wa mkewe, Irene Uwoya, aliponaswa hotelini na mwamuziki, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.



Habari za kuzimia kwa Ndiku, zimewekwa kweupe na Uwoya mwenyewe, aliyesema: “Maskini Ndikumana wangu, baada tu ya kusoma habari ya mimi na Diamond alianguka na kuzimia.”
Kwa tafsiri, Uwoya anamsikitikia mume wake kuanguka na kuzimia, upande wa pili anajuta kumfahamu Diamond, kwani ndiye aliyemsababishia majanga yote.
Hivi sasa, Ndiku yupo Rwanda, alitimka nchini baada ya kusoma habari ya Uwoya na Diamond kunaswa hotelini, ila kabla ya kuondoka, alitamka rasmi kuvunjika kwa ndoa yao.
Habari ya kuvunjika kwa ndoa, ilitoka kwa Uwoya mwenyewe ambaye alimweleza mwandishi wetu siku Ijumaa Wikienda, lilipodondosha ‘jiwe’ hilo mtaani. Uwoya alisema: “Na ndoa yenyewe imevunjika asubuhi ya leo, kila kitu kimeharibika.”
KWELI ANAJUTA KUMFAHAMU DIAMOND
Uzungumzaji na hata sauti, ni dhahiri Uwoya hataki tena kumsikia Diamond, kutokana na ukweli kuwa ‘brazameni’ huyo, amemharibia kila kitu, ikiwemo kuipeleka kaburini ndoa yao.
Yafuatayo ni mahojiano kati ya Uwoya na mwandishi wetu;
MWANDISHI: Habari za kazi?
UWOYA: Salama tu. 
MWANDISHI: Vipi shemeji yetu hajambo?
UWOYA: Shemeji gani? (anatukana) mume wangu ameniacha kisa stori ya Diamond.
MWANDISHI: Duh, imekuwaje tena jamani?
UWOYA: Alipoona stori ya mimi kuwa hotelini na Diamond, aliumia sana. Akaanguka na kuzimia.
MWANDISHI: Shida ilikuwa habari ya Diamond au mgogoro ndani ya ndoa?
UWOYA: Alipoona ile habari kwenye gazeti alianguka ghafla, akazimia kisha alipozinduka akarudi kwao. Ameamua kuniacha sijui kama atanirudia. 
MWANDISHI: Pole sana, kwa hiyo familia yako inasemaje kuhusu hilo?
UWOYA: Familia yangu imenitenga kwa sasa.
MWANDISHI: Pole sana Uwoya.
UWOYA: Haina haja. Andikeni tu, mume wangu amenitosa rasmi.
MWANDISHI: Kwani amekupa talaka ndugu? Maana ndoa haiwezi kuharibika kirahisi.
UWOYA: Mimi na wewe hatutaniani, nakwambia ndoa yangu haipo tena. 
MWANDISHI: Lakini shemeji yetu anakupenda sana.
UWOYA: Unataka kuandika hayo? Ukweli familia yangu haitaki kabisa kusikia habari za Diamond.
MWANDISHI: Kwani magazeti ya Global hayajasaidia kurejea kwa ndoa yako?
UWOYA: Mliandika habari nzuri ya ndoa yetu, tukarudiana, mlinisaidia sana na familia ilifurahi kuona hayo kwa wakati huo.
MWANDISHI: Sasa nani wa kulaumiwa juu ya ndoa yako?
UWOYA: Mimi niko ‘siriaz’, nimeachwa.
MWANDISHI: Ok, asante ndugu.
UWOYA: Asante, Mungu atawalipia tu.
KUHUSU DIAMOND NA UWOYA
Machi 25, mwaka huu, Diamond na Uwoya, walinaswa na kamera za Global Publishers Ltd (nyumba kubwa ya magazeti pendwa), kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Ijumaa Wikienda ambalo ni gazeti ndugu na hili, lilianika kila kitu, huku likiwa na ushahidi wa kutosha jinsi Diamond na Uwoya, walivyolala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, wakiingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.

No comments:

Post a Comment