Monday, April 29, 2013

ANAETAJWA KUWA MRITHI WA JOSE MOURINHO

Kocha wa Paris St Germain Muitaliano Carlo Ancelotti ametajwa kuwa mbioni kurithi nafasi itakayoachwa wazi na Jose Mourinho kama kocha wa Real Madrid ambapo inasemekana Ancelotti tayari ameingia kwenye makubaliano yasiyo rasmi na atachukua nafasi hiyo siku chache baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Moja ya tetesi ambazo zimejaza kurasa za magazeti yenye habari za michezo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni ile inayohusu Jose Mourinho kuondoka kwenye klabu ya Real Madrid ambako amekuwa hana mahusiano mazuri na baadhi ya watu akiwemo nahodha Iker Cassilas na baadhi ya viongozi.

Carlo Ancelotti kwa upande wake amekuwa akihusishwa na taarifa za kufukuzwa kazi na mabosi wa Paris St Germain ambao wamekuwa hawafurahishwi na aina ya soka linalochezwa na klabu hiyo pamoja na usajili mkubwa ambao imeufanya, uongozi wa Real Madrid unaamini kuwa Ancelotti ana uzoefu na uwezo wa kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ulaya kama alivyowahi kufanya mara mbili akiwa na Ac Milan pamoja na Juventus ambayo aliiongoza kufika fainali ya michuano hiyo.
Kama Real Madrid itatolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa ambako iko nyuma kwa mabao manne baada ya mchezo wa kwanza, mwisho wa Jose Mourinho utakuwa umekaribia kwani atakuwa ameshindwa kuipa klabu hiyo mafanikio iliyotarajia ya ubingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 11.

Monday, April 22, 2013

MAOFISA MAGEREZA MKOANI KAGERA WATUNUKIWA VYEO

 Mkuu wa magereza kagera Yusuph Kimanji akimvalisha cheo mmoja wa maofisa wa magereza.

Sunday, April 21, 2013

HARUSI YA MDAU MOHAMED KHASIM ILIKUWA YA KIMA TAIFA...

 bwana harusi na bibi harusi wakifungua sherehe

 mr&mrs simba wakipiga picha ya pamoja

 wadau wakijiandaa kuingia ukumbini
 bwana harusi na bibi harusi wakiusakata mziki
 full shangwe kwa wana kamati

 mdau mr&mrs ibrahim wakipata picha ya pamoja

 mr&mr mohamed khasim(bwana na bibi arusi)

dada rukia (dada wa bwana harusi)

 wana kamati wakitokelezea

 wanakamati wakipanga mikakati na mc

 maharusi wakipiga picha ya pamoja

 mh erenest nyambo

 mr jamco (mwenyekiti wa kamati)
 waalikwa wakipiga picha ya pamoja
 wazazi wa mohamed khasim
lulu akiongoza msafala wa maarusi
 mr athumani akitokelezea
 bata za kutosha
kweli harusi ilikuwa ni ya kitofauti, kitu ambacho ni cha kujivunia kuanzia kwa bwana harusi alivaa suti ya kitofauti na inavyo semekana aijawai kutokea apa nchini japo suti hiyo ilikuwa made in Tanzania wadau walijifunza mengi kupitia hilo, siwez kuyasema yote hiyo ndo harusi ya bwana na bibi mohamed khasim. mungu ibaliki tanzania wabariki mr na mrs khasim katika ndoa yao wabaliki na wadau wote amen

Saturday, April 20, 2013

ROSE NDAUKA AWATEGA MADENTI

Stori:Denis Mtima

STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye ‘industry’ ya filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni alitinga kivazi kifupi ambacho kiliwachengua madenti wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ambao walibaki kumkodolea macho mwanzo mwisho.

Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za…

Stori:Denis Mtima
STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye ‘industry’ ya filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni alitinga kivazi kifupi ambacho kiliwachengua madenti wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ambao walibaki kumkodolea macho mwanzo mwisho.

Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.
Kutokana na kivazi hicho alichokivaa na mvuto alionao staa huyo, baadhi ya madenti wakware walionekana wakipoteza usikivu wa hotuba ya mgeni rasmi na kubaki kumtazama.
“Mh! Rose ni mzuri jamani uongo dhambi, nilikuwa nikimuona katika runinga leo nimemuona live daaah!” alisikika denti mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.