Tuesday, July 16, 2013

MACHANGU" TUNAENDELEA KUJIUZA MWEZI MTUKUFU ILI TUPATE HELA YA FUTARI"


OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na mapaparazi wa Global Publishers inazidi kufichua ‘madudu’ kwenye jamii, safari hii imekutana na machangu ambao wamecharuka kuendeleza biashara hiyo kwa kisingizio cha kutafuta fedha za kununulia futari.

‘Askari’ wa OFM, wiki iliyopita alifanya uchunguzi katika viunga mbalimbali maarufu kwa biashara hiyo na kukuta machangudoa wakifanya biashara yao kama inavyokuwa katika miezi ya kawaida.
Maeneo ambayo yalionekana kushamiri zaidi kwa biashara hiyo ni Barabara ya Mwananyamala Hospitali, American Chipsi, Makaburi ya Kinondoni, Viwanja vya Leaders Club, Taasisi ya Moyo, Jolly Club (Masaki), Hospitali ya Agha-Khan, New Maisha Club (Masaki) na Coco Beach.

Idadi kubwa ya wadada hao walipohojiwa na paparazi wetu, walisema wanaendelea na biashara hiyo kwa kuwa ndiyo waliyoizoea kutafutia kipato na wakiiacha, watakufa kwa njaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Ili kujiridhisha kwa data, paparazi wetu alijifanya mteja na kukutana na machangu wa Makaburi ya Kinondoni ambao walidai wanapenda waitwe ‘scraper’ au vyuma chakavu pasipo kufafanua zaidi, bahati mbaya wakashtukia mchezo:
Changudoa: “We kaka mbona unatuzingua? We ulivyokuja si ulijifanya mteja, kumbe paparazi, sisi hatuwezi kuacha kujiuza kwa kuwa ndiyo kazi tuliyoizoea, sasa tukikaa nyumbani tutapata wapi futari?” alihoji mmoja wa machangudoa.
Paparazi: “Hivi ni kweli nyie mnafunga?”

Changudoa: “Wewe tumia ubongo na maswali yako yanayotia njaa, hata kama sisi tunafunga au hatufungi tuna watu wanaotutegemea majumbani kwetu kuwatafutia futari, sasa tusipohangaika itakuwaje?”
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu waliozungumza na Ijumaa Wikienda, walionesha kukerwa na tabia hiyo na kulaani vibaya kwani mwezi huu ni maalum kwa ajili ya kumrudia mwenyezi Mungu na kuacha dhambi.

No comments:

Post a Comment