Thursday, July 18, 2013

AGAPE TELEVISHENI WAZINDUA VING’AMUZI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Agape Televisheni, Andy Fernandes (katikati) akielezea umuhimu wa kutumia ving’amuzi hivyo. Kulia ni Waziri Mbalawa na kushoto ni Mkurugenzi wa Agape Televisheni Network, Dr. Anne Fernandes.
Waandishi wa habari wakiwa kazini.
Mbalawa akizindua king’amuzi hicho.
…Akikiunganisha na luninga.
Mbalawa akimpa king’amuzi Shehe Alhad.
WAZIRI wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbalawa, leo amezindua king’amuzi kipya cha TING HD ambacho kipo chini ya kituo cha luninga cha Agape.
Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum, na mashehe wengine na wachungaji wa makanisa mbalimbali.
Katika uzinduzi huo Mbalawa alieleza umuhimu wa kutumia ving’amuzi hivyo vyenye uwezo wa HD ‘High Definition’ na kusema ndiyo ving’amuzi pekee vyenye ubora wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment