Saturday, August 24, 2013

MIJIMAMA: WANAUME WANATUPENDA SISI MABONGE




Na Waandishi Wetu
MAKUBWA! Madogo yana nafuu! Wanawake wenye maumbile makubwa wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao jijini Dar, wamefunguka kwamba wanaume wamekuwa wakiwapenda kwa sababu ya ubonge wao

Mijimama hiyo ilitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati ikizungumza na paparazi wetu aliyekuwa katika oparesheni maalum ya kuhojiana nao ili kujua kinachowafanya wajihusishe na biashara hiyo inayohatarisha maisha yao.

Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Zainabu anayefanya biashara hiyo maeneo ya Sinza Afrika Sana, alisema umbo lake limekuwa likiwadatisha wanaume kibao.

“Kaka si unaiona hii shepu yangu, hapa kuna mwanaume anayeweza kunipita na kwenda kwa wale vimbaumbau,” alisema Zainabu huku akimuonesha paparazi wetu wasichana wembamba waliokuwa mbele yao



Mwanamke mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Sara Mashauzi, aliyekuwa katika mawindo ya wanaume wakware na Zainabu alisema: “Mimi nilianza haya mambo baada ya kuachana na mume wangu, sasa kila ninakopita wanaume wakiniona tu huanza kunipigia miluzi na wengine kuniita, sista… sista… hongera…, nikaamua kujiuza ili nipate kipato kwani maisha yalibana sana.”
Sara aliongeza kuwa, wanaume wengi anaotoka nao wamekuwa wakimsifia kwa umbo lake ‘pana’ na kudai kwa siku huwa hakosi shilingi 50,000 na siku nyingine anapata hadi 80,000.

Karibu wanawake wote mabonge waliozungumza na paparazi wetu maeneo ya Kinondoni, Buguruni, Manzese na Oysterbay ambako biashara hiyo imeshamiri walidai maumbo yao yamekuwa yakipendwa sana na wanaume hususan waume za watu.
Paparazi wetu alipomuuliza Sara, Zainabu na mwenzao aliyejitambulisha kwa jina la Sikitu kwamba hawaoni kama wanaharibu soko la wenzao wembamba, kama vile waliambiana jibu wakasema watajiju!



Baadhi ya madadapoa wembamba waliozungumza na paparazi wetu, waliwafungukia majimama hao na kudai wamewaharibia soko lao na kusababisha wajiuze kwa promosheni.

Gazeti hili linakemea tabia hiyo chafu na isiyofaa katika jamii na kuviomba vyombo husika kupambana na kuwasambaratisha wasichana hao. Mhariri.

No comments:

Post a Comment