Monday, February 3, 2014

Zogo baada ya Msikiti kuvamiwa Kenya



Polisi na vijana waisilamu wamekabiliana Mombasa baada ya tukio la Jumapili
Vijana walioghadhabishwa na tukio la polisi kuvamia msikiti mmoja unaotumiwa na wahubiri wanaosemekana kuhubiri itikadi kali za kiisilamu mjini Mombasa,Pwani ya Kenya, wamekabiliana na polisi kwa siku ya pili leo.
Duru zinasema kuwa Maafisa wa usalama wanakutana kujadili matukio ya Jumapili mjini Mombasa ambapo polisi waliwakamata vijana katika msikiti wa Musa .
Waliokamatwa walifikishwa mahakamani kujibu makosa ya kujihusisha na ugaidi.
Msako wa polisi ulisababisha vifo vya watu watatu akiwemo polisi mmoja huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Polisi walichukua muda wa masaa tatu kuendesha msako, katika msikiti wa Musa mtaani Majengo baada ya kupata habari kuwa mkutano wa vijana kuhusu jihad ulikuwa unaendelea ndani ya msikiti huo.
Zogo lilianza baada ya vijana waliokuwa ndani ya msikiti huo unaohushwa na marehemu Aboud Rogo kuzuia polisi kuingia ndani. Watu watatu waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati polisi wakifanikiwa kuwakamata vijana karibu miamoja.
Miongoni mwa waliokamatwa alikuwa mwanawe marehemu Rogo aliyesema kuwa wakati walipokamatwa kulikuwa na bunduki 18 ndani ya msikiti huo na kuwa alihadaiwa kuhudhuria mkutano huo.
Taarifa zinasema kuwa mkutano huo wa vijana uliandaliwa kupitia mitandao ya kijamii huku vijikaratasi vikisambazwa mjini humo kuwaalika watu.

THAMANI YA MALI ALIZOKUWA ANAMILIKI HAYATI NELSON MANDELA ZATANGAZWA


Mandela alifariki mwezi Disemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 95
Hayati Nelson Mandela, aliachia familia yake mali yake yenye thamani ya dola milioni 4.1.
 Sehemu ya mali hiyo pia itatolewa kwa chama tawala ANC, wafanyakazi wake wa zamani na shule kadhaa ambako alisomea.

Hayo ndio yalikuwa mapenzi ya Mandela ambayo yalikuwa kwenye wasia wake uliosomwa hadharani kwa familia nzima.
 Afisaa Dikgang Moseneke aliyekabidhiwa jukumu la kusoma wasia huo wenye kurasa 40 na kuhakikisha unatekelezwa ,alisema hapajakuwa na pingamizi zozote kuhusu yaliyomo kutoka kwa familia ya Mandela.
 Wafanyakazi wa karibu wa Mandela watapata randi 50,000 kila mmoja. Shule ambazo Mandela alisomea zitapata randi laki moja kila shule.
 Hayati Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95.
 Familia ya Mandela tangu hapo imekuwa ikizozana kuhusu urithi wa hayati Mandela na kuna hofu kuwa huenda wasia huu ukasababisha mgogoro mwingine kuhusu mali hiyo.
 Mali ya hayati Mandela inajumuisha nyumba na hakimiliki za vitabu ikiwemo kimoja kuhusu maisha yake kwa jina ''Long walk to freedom'' 

RAIS KIKWETE:MBOWE ANAKOSA UWEZO, JAMBO LA WENGI HALITAAMULIWA KWA NGUMI


Rais Kikwete: Mbowe anakosa uwezo, jambo la wengi halitaamuliwa kwa ngumi
Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 37 ya CCM alimwambia Mheshimiwa Mbowe kuwa nashanganzwa na kauli yake kwamba isipopatikana Serikali tatu atapambana kwa ngumi na mateke mpaka ipatikane.

“uliona wapi jambo la wengi likiamuliwa kwa ngumi?” aliendelea Kikwete kwa kusema “hakuna katiba ya nchi dunia iliyopatikana kwa kutumia ngumi na hata Mbowe akiamua kupigana sina hakika kama atamshinda John Komba au Mheshimiwa Mnyika kumpiga Mheshimiwa Missanga”.

Bunge la katiba ndilo litakalopitisha aina ya katiba tunayoitaka kwa niaba yetu na lina uwezo wa hata kuja na rasimu ya katika yao tofauti kabisa na ya sasa na ikawa halali.

Alimalizia kwa kusema “katiba mpya ikikwama tutaendelea na katiba ya sasa”

Sunday, February 2, 2014

UN:Milioni 3.7 wana njaa S.Kusini

UN inasema kuwa vita vinaendelea licha ya mkataba wa amani kutiwa saini
Umoja wa mataifa unakadiria kwamba takriban watu millioni 3.7 nchini Sudan kusini wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.
Mratibu wa maswala ya kibinaadamu katika umoja huo Toby Lanzer ameiambia BBC kwamba mzozo huo ulioanza mwezi Disemba mwaka jana umeharibu masoko pamoja na maisha ya kawaida ya watu, mbali na kusababisha hali mbaya ya kibinaadamu kwa thuluthi moja ya idadi ya raia.
Na ili kuzuia Janga ,amesema kuwa umoja wa mataifa unahitaji dola millioni 1.3 pamoja na mazingira yalio salama ili kutekeleza wajibu wake.
Maelfu ya raia wamepoteza maisha yao katika vita hivyo ambavyo umoja wa mataifa unasema vinaendelea licha ya kutiwa saini kwa mkaaba wa kuvisitisha ju
UN inasema kuwa vita vinaendelea licha ya mkataba wa amani kutiwa saini
ma moja lililopita.

KIKONGWE AKAMATWA CHUMBANI KWA MTU AZANIWA KUWA NI MCHAWI-PICHA



Hili ni tukio lilitokea huko Bukoba ambalo linamhusisha Kikongwe mmoja ambaye jina lake bado halijapatikana kukutwa chumbani kwa mtu huku akiwa mtupu chumbani kwa mtu.
25Mpaka sasa bado haijajulikana kama ni Kigarura au pengine alipata matamani ya mwili akaona pengine chumba kile kingemfaa kumpatia msaada wa mambo yake.
28Bibi Kizee huyo anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 70,ambapo amekamatwa alfajiri ya leo January 31 hata hivyo polisi wamefanikiwa kumnusuru na kifo baada ya kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi.
30Mashuhuda wa mwanzo wanadai walimkuta bibi huyo akitapatapa bila kujua nini la kufanya huku akiwa mtupu na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kilichotafsiriwa kwamba pengine bibi huyo anaweza kuwa mchawi,huku wengine wakisubiri taarifa ya polisi na wengine wakisema huenda bibi huyo alipatwa na matamanio ya kimwili.

SIRI 7 ZA KUVUNJA NDOA NA MBUNGE MZEE!


YULE ‘hendsam’boi’ Michael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) na miezi michache mbele ndoa ikavunjika, ameibuka na kuanika siri 7 zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar, juzi,…
Stori: Imelda Mtema na Ojuku Abraham YULE ‘hendsam’boi’ Michael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) na miezi michache mbele ndoa ikavunjika, ameibuka na kuanika siri 7 zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar, juzi, Michael alibainisha mambo hayo huku akisema anajuta kwa tukio lile ambalo bado halijamtoka kichwani hadi sasa.
Michael Christian‘hendsam’boi’, alipotua ndani ya  Ofisi za Global jijini Dar.
SIRI YA KWANZA
Kijana Michael aliianika siri ya kwanza kwamba ni kuchekwa na marafiki zake wa Bagamoyo mara baada ya kugundua amefunga ndoa na mbunge huyo ‘mzee’.
“Marafiki zangu walianza kunicheka, walisema nimefunga ndoa na mbunge mzee, mama mtu mzima. Nikaanza kujisikia vibaya jambo ambalo sikulipenda hata kidogo,” alisema kijana huyo ambaye ni yatima.

SIRI YA PILI
Akizungumza kwa hisia kali, Michael aliye na taaluma ya uuguzi, aliiweka wazi siri ya pili ya kuamua kuivunja ndoa yake na mheshimiwa huyo kuwa ni kitendo cha kutokuwepo kwa tangazo la ndoa la siku 21 kama sheria ya nchi inavyotaka.
Kuna kifungu cha sheria kinachotaka wachumba wanapotaka kufunga ndoa kutolewa tangazo la siku 21 kwenye mamlaka za kufungisha ndoa hiyo ili kama mmoja wa wahusika ana ndoa inayoishi (halali) aweze kuwekewa pingamizi la kufungishwa ndoa.
SIRI YA TATU
Kijana huyo aliendelea kwa kuifunua siri ya tatu kuwa ni kitendo cha kufungishwa ndoa bila kuwepo na mashahidi wa pande zote mbili (matroni na patroni) walioandaliwa zaidi ya kuitwa papohapo.
Alimtaja kwa jina moja Mchungaji Mtetumo wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’ kuwa ndiye aliyesimamia kufungwa kwa ndoa hiyo, Septemba Mosi, 2011 ndani ya ofisi huku milango ikiwa imefungwa.
Alisema pia kwamba, suala la ndoa aliligundua siku hiyohiyo baada ya kufika kwenye kanisa hilo ambapo maandalizi mengine yote yalishafanyika akiwa hajui.

SIRI YA NNE
Siri zilizidi kubanjuliwa, Michael alisema sababu ya nne ambayo pia ilimsukuma kuamua kubatilisha ndoa yake na mama Kasikila ni baada ya kubaini kwamba, hataweza kupata uzao kwa mke huyo kwa sababu ana watoto wakubwa kiumri kuliko yeye.
“Nilijua sitapata watoto, hakukubali kuzaa na mimi kwa sababu tayari ana watoto wakubwa, mimi mdogo, ingekuwa vigumu. Kifupi haikuwa ndoa halali kwangu,” alisema kijana huyo.

SIRI YA TANO
Michael: “Alianza kunibana sana, kila hatua ya miguu yangu alitaka kujua inakwenda mpaka wapi! Hii hali nikaiona inanipiga pingu, nikagundua kuwa kumbe mimi sijaoa, bali nimeolewa. Yule mama alinioa mimi, si kwamba mimi nilimuoa yeye, nikasema ili niwe na amani ya moyo ni lazima ndoa ivunjike.”

SIRI YA SITA
Kijana huyo hakuona sababu ya kubakiza siri hata moja, akaendelea kuzianika:
“Jambo jingine ambalo pia lilichangia kuamua kuivunja ndoa ile ni baada ya kukumbuka historia ya kukutana kwetu.
“Wakati nipo Hospitali ya Bagamoyo na yeye akiwa pale kama muuguzi mkuu, tulizoeana. Kuna siku aliniita kwake akasema anasafiri anaomba nimwangalizie nyumba, nilikuwa na rafiki yangu tukawa tunalala pale mpaka aliporudi.
“Kuzoeana kuliendelea, mwishowe tukawa wapenzi mpaka ndoa. Nilipokumbuka hivyo tu nikagundua kuwa aliniingiza mapenzini kwa hila au mbinu, hilo pia sikulipenda,” alisema Michael.   

SIRI YA SABA
Michael alisema sababu ya saba ambayo pia ilimshinikiza kuivunja ndoa hiyo ni kupwaya ndani ya nyumba.
Alisema kutokana na umri wake, ndani ya nyumba alijiona ni mtoto na si mume kama wanaume wengine walivyo.
“Hata uwezo wangu wa mawazo kwake haukuwa wa mume na mke, ni wa mtoto na mama. Kifupi haikuwa ndoa halali,” alisema.

SIKU ALIPOIVUNJA NDOA
Kijana huyo alisema ndoa yake na mheshimiwa huyo aliivunja mbele ya Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God, Dk. Getrude Rwakatare walipokwenda kusuluhishwa ili waende wakaishi kwa amani.
Alisema kabla ya usuluhishi alimfungukia mama Rwakatare kuhusu manyanyaso anayoyapata ndani ya ndoa hiyo ndipo aliposimama na kuivua pete kisha kuitupa chini huku akisema katu hawezi kurudi kwa mkewe huyo na ndoa imevunjika, akaondoka zake.

ANATAKA KILIO CHAKE KIFIKE KWA JK
Kijana Michael alisema kilio chake kikubwa kwa sasa ambacho angependa kifike hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ni kitendo cha mkewe huyo kuzuia vyeti vyake ambavyo vingemsaidia kutafutia kazi sehemu mbalimbali.

“Amezuia vyeti vyangu vyote, kila nikimwambia navitaka nikienda ananifanyia visa, nawaomba Watanzania wanisaidie kwa hili.
“Mimi kwa sasa nataka vyeti tu, sitaki cha ndoa wala nini? Lakini hataki kunipa,” alisema Michael.

MSIKIE MBUNGE SASA
Akijibu tuhuma hizo, Mheshimiwa Kasikila alikiri kuwa na vyeti vinavyolalamikiwa na mumewe huyo, lakini alikanusha kwa nguvu zote juu ya maneno kuwa yeye ameoana na mtoto mdogo, akirejea vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinavyomtaja mtoto kama ni mtu wa namna gani.
Mbunge: “Mwandishi, unafahamu mtoto kwa katiba yetu ni mtu wa namna gani?”
Mwandishi: “Ni mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane.”
Mbunge: “Sasa Michael ni mtoto? Ana miaka 28 unamuita mtoto?”

AWAWEWESEKEA WANASIASA
Alisema anajua suala hilo lina shinikizo la kisiasa, kwani hivi karibuni baadhi ya wanasiasa walikwenda jimboni kwake wakiwa na nakala ya gazeti moja lililoandika habari zake na kijana huyo na kuwaambia wapigakura wake kuwa mbunge wao ameoa kitoto, lakini wapigakura wake waliwapuuza kwa kuwaambia hilo haliwahusu kwani wanachojua anawawakilisha vizuri bungeni.
“Kama kweli ninyi mnampenda huyo Michael, muelekezeni sehemu sahihi ya kwenda kupeleka madai yake. Ngoja nikupe mfano, mimi nikiwa wizara ya afya, mtu akija na malalamiko kuhusu pembejeo za kilimo, kwa kumsaidia, nitamuelekeza aende wizara ya kilimo, kwa kuwa pale (afya) siyo sehemu yake, sasa nyinyi muelekezeni huyo sehemu sahihi ya kupata haki yake, siyo huko magazetini,” alisema mama huyo.

LIBYA MABINGWA CHAN 2014

TIMU ya taifa ya Libya imetwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2014 baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana Jumamosi Uwanja wa Cape Town.
Ushindi huo ni sawa na Libya kulipa kisasi kwa Ghana baada ya kufungwa kwa penalti 7-6 miaka 32 iliyopita kwenye fainali ya Kombe