*Awaonya wanaomwita msaliti
*Dk. Slaa aibua mapya
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, aliyesimamishwa
uongozi asema atakichafua chama hicho kama ataendelea kuitwa msaliti.
Hatua hiyo, imekuja baada ya Mwigamba
kukiri hadharani kusambaza waraka unaowatuhumu viongozi wa chama hicho
katika mtandao wa Jamii Forum (JF), akitumia jina la Maskini Mkulima.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mwigamba aliwaonya
viongozi wa Chadema wanaomwita msaliti. Alisema kama wanataka awe
msaliti, yupo tayari kumwaga mambo yote hadharani, tena kwa ushahidi
usio na shaka hata kidogo.
Mwigamba, aliyejiunga na Chadema
mwaka 2004, akiwa mwanachama wa kawaida, alisema akiwa makao makuu mjini
Dar es Salaam kama mhasibu mkuu wa chama, ndipo alipoanza kutambua
udhaifu mkubwa wa kiuongozi ndani ya chama chake.
“Niliondoka pale makao makuu kwa
mizengwe, kiongozi mmoja mkubwa kabisa alinifukuza kazi kwa kunipigia
simu, tena baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa Fedha,Anthony Komu
akiwa nje ya Dar es Salaam na kumwagiza anifukuze,” alisema Mwigamba.
Alisema kwa bahati mbaya, udhaifu huo
umeshindwa kushughulikiwa na vikao rasmi vya chama, kwani yeyote
anayejaribu kukosoa ama kuhoji iwe ndani ya vikao rasmi ama nje,
hutangazwa kuwa ni msaliti.
Alisema kutokana na hali hiyo, ni
wajumbe wachache ndani ya Chadema, hasa kwenye Kamati Kuu, ambao
wanaweza kusimama kidete na kukosoa uongozi.
Aliwataja wajumbe hao, kuwa ni Dk.
Kitila Mkumbo, Profesa Mwesiga Baregu, Mzee Shilungushela na marehemu
Magadula Sherembi kabla hajafariki dunia.
Hata baada ya kuondolewa Aprili,
mwaka jana, alirejea Arusha na hakuwahi kujitokeza kwenye vyombo vya
habari ama mitandao kuzungumzia tatizo la viongozi na uongozi ndani ya
chama.
“Matatizo yaliyomo ndani ya chama
ambayo wanachama wa kawaida wanaokiamini chama na viongozi wake
wangeyasikia, hakika wangeweza kukata tamaa.
“Nimefanya hivyo kwa mapenzi na kwa
maslahi ya chama changu, sasa kama viongozi wenzangu wanataka niwe
msaliti basi waniambie hata leo nimwage ambayo yote hadharani, tena kwa
ushahidi usio na shaka hata kidogo.
Huyu ni staa wa mpira aitwaye Zlatan Ibrahimovic akiwa katika
wakati mgumu baada ya mzigo wake kuvimba akiwa uwanjani…
Taarifa zinaarifu kuwa, mzigo huo ulivimba baada ya mchezaji mwenzake kumkumbatia kwa nyuma..
NCHI za Tanzania na Burundi, kwa mara
nyingine zimetengwa na wenzao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
baada ya marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana mjini Kigali jana.
Marais hao walitarajia kujadili namna ya kuimarisha Jumuiya ya Afrika
Mashariki kupitia uimarishwaji wa miundombinu, uchumi, biashara pamoja
na kuweka mikakati ya shirikisho la kisiasa.
Kitendo cha kuziacha Tanzania na
Burundi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kinazidi
kutia shaka mtangamano wa jumuiya hiyo.
Nchi hizo mbili zimeshaeleza
kusikitishwa na muungano wa nchi hizo tatu, ambao zimesema unakwenda
kinyume cha makubaliano na mkataba wa EAC.
Katika mkutano huo, marais hao, Paul
Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya,
pamoja na mambo mengine, walitarajia kusaini makubaliano ya kuanzisha
kituo kimoja cha kukusanya ushuru kinachotarajia kurahisisha uchukuzi wa
bidhaa kutoka Mombasa nchini Kenya, Uganda hadi Rwanda.
Aidha Sudan Kusini ilialikwa ikiidhinishwa kama mshirika katika kikao hicho.
Mkutano huo unakuja baada ya ule
uliofanyika mjini Kampala, Uganda, Juni mwaka huu na mwingine
uliofanyika Mombasa, Agosti, ambako viongozi hao watatu walipendekeza
kupanuliwa kwa Bandari ya Mombasa, ili kuwezesha uharaka wa bidhaa
kupitishwa katika kuhudumia kanda nzima.
Mkutano mwingine wa marais wa nchi 15
za Afrika, ikiwamo Tanzania, utafanyika leo nchini hapa, katika
kongamano la siku nne ambalo linatarajiwa kuweka kipaumbele kwa
uimarishwaji wa huduma za internet katika mataifa hayo.
Kwa mujibu ya waandaaji, zaidi ya
wajumbe 1,500 watahudhuria mkutano huo, chini ya uenyeji wa Rais Paul
Kagame na Dk. Hamadoun I. Toure, Katibu Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa
Mawasiliano ya Kiteknolojia (ITU).
-Mtanzania
Mtu mmoja jijini Mwanza anadaiwa kukamatwa na kiganja cha mtu akiwa anajiandaa kumuuzia mteja kwa sh million 100.
Washukiwa walikamatwa jana karibia na uwanja wa ndege wa Mwanza wakifanya biashara hiyo haramu....
Baada ya upekuzi wa kina, mteja
alikuwa ana milioni 100 na mganga alikutwa na kiganja cha
binadamu ambacho kilikuwa kibichi kikitoa damu.
Kiganja hicho kilikuwa kimevishwa tunguri na nywele za binadamu.
JESHI la Polisi nchini limewafukuza
kazi askari wake 56 katika kipindi cha mwaka mmoja, kutokana na makosa
ya kuomba na kupokea rushwa pamoja na utovu wa nidhamu.
Kamishna msaidizi wa jeshi hilo,
Patrick Byatao, alisema hayo jana alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya
mambo mbalimbali hususan masuala ya nidhamu kwa askari wake katika
warsha ya siku maalumu ya polisi iliyofanyika mjini Bukoba.
Alisema kuwa askari waliofukuzwa ni
kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambao wamekutwa na tuhuma za utovu
wa nidhamu ikiwemo kuomba rushwa kwa wananchi. Kwa kipindi cha mwaka
2012, waliwafukuza askari 35 na mwaka huu 21.
Kwa mujibu wa Byatao, wapo baadhi ya
askari ambao wamekuwa wakitoa visingizio vya kuomba rushwa kwa sababu
mishahara yao ni midogo na haitoshelezi mahitaji yao.
Alisema ni heri askari wa aina hiyo
wakaacha jeshi, vinginevyo wataendelea kuchukuliwa hatua kama
hawatafuata masharti ya kazi yao.
Akitoa mada juu ya kuimarisha maadili
ndani ya jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka makao makuu,
Andrew Makungu, alisema wameanzisha mkakakati wa kudhibiti vitendo vya
ukiukwaji maadili kwa askari wake ikiwemo rushwa.
Alitaja maeneo lengwa kuwa ni chumba
cha kupokea taarifa za mashitaka, usalama barabarani na upelelezi wa
makosa ya jinai. Bado juhudi zinaendelea ili kuboresha maeneo mengine.
Makungu alisema ubia wa kiutendaji wa
jeshi hilo umekuwa ukiimarika kila siku baada ya sehemu kubwa ya jamii
kutambua nafasi yao katika jukumu hilo.
Alisema mambo hayo yanaonekana
kutokana na wananchi kufanya ulinzi wa maeneo yao, kuchangia rasilimali
kwa jeshi, kutoa taarifa sahihi za uhalifu, kujenga vituo vya polisi na
kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi. Hadi sasa viko vikundi 5,344
nchi nzima huku Mkoa wa Kagera ukiwa na 431.
Naye mgeni rasmi katika warsha hiyo,
Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa
wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, alisema kuwa Jeshi la Polisi
limekuja na mkakati wa polisi jamii/ulinzi shirikishi unaoelekeza kuwapo
kwa mashauriano, majadiliano ya kiutendaji yanayosisitiza uwepo wa
maadili katika kazi, ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa ndani ya jamii.
Katika mahojiano maalumu na timu ya
waandishi wa Mwananchi na The Citizen jana, Graf alisema kuwa Serikali
ya Tanzania inapaswa kusaini mkataba wa kimataifa wa kubadilishana
taarifa za masuala ya usimamizi wa fedha na kodi ili kuweza kujua ni
kina nani wameweka fedha nchini kwake na kunufaika na kodi.
Graf, ambaye alikuwa katika ziara ya
kikazi nchini, alisema kuwa hivi karibuni Serikali ya Uswisi ilisaini
mkataba wa kimataifa wa kubadilishana taarifa kuhusu masuala ya fedha,
ambao unajulikana kwa lugha ya Kiingereza kama `Convention on Mutual
Administrative Assistance in Tax Matters’.
Alisema ikisaini mkataba huo ina maana itasaidiwa na Serikali ya Uswisi kupata fedha zilizofichwa na Watanzania.
“Serikali ya Tanzania inatakiwa
kuweka mkakati wa kisheria utakaotengeneza mazingira ya kubadilishana
taarifa za fedha na mataifa mengine. Kwa jambo hilo hata Serikali ya
Uswisi inaweza kusaidia katika kupatikana kwa fedha zilizofichwa,”
alisema Graf, ambaye anaongoza Serikali ya Uswisi kwani kwa kawaida Rais
wa Bunge ndiye pia kiongozi wa taifa hilo.
Graf alisema kwa sasa itakuwa ngumu
kwa Tanzania kupata fedha hizo kwani haijasaini mkataba wa kimataifa wa
kubadilishana taarifa za fedha na mataifa mengine.
Alieleza pia katika miaka ya karibuni
Serikali ya Uswisi imeandaa muswada wa sheria wa kubana fedha
zilizopatikana kwa njia za kifisadi na kufichwa katika benki za Uswisi.
Graf alisema sheria hiyo ikipita itaruhusu Serikali ya nchi hiyo
kutaifisha fedha ambazo zimepatikana kwa njia haramu na kufichwa katika
benki za huko.
Muswada huo unaoitwa kwa lugha ya
Kiingereza `Freezing and Restitution of Assets of Politically Exposed
Persons obtained by Unlawful Means Bill’ ulisomwa kwa mara ya kwanza
kwenye Bunge la nchi hiyo mwezi Mei, mwaka huu.
Graf alisema faida nyingine ya Tanzania kusaini mkataba huo ni kuwa, itaweza kuwatoza kodi Watanzania hao walioweka fedha huko.
Alifafanua kuwa siyo fedha zote
zinazowekwa kwenye benki za Uswisi kuwa ni haramu kwani kuna nyingine
zimepatikana kihalali, lakini zinaweza kutozwa kodi.
“Tanzania inakosa kodi kutokana na
fedha zilizohifadhiwa na Watanzania wenye akaunti kwenye benki za
Uswisi,” aliongeza Graf, ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo
Novemba 26, 2012 na kutakiwa kukaa madarakani kwa mwaka mmoja.
Graf alisema pia fedha za kodi zingeisaidia Tanzania kugharimia sekta mbalimbali za maendeleo.
Zito aitupia lawama Serikali
Naye Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto
Kabwe, ambaye yuko nchini Uswisi akifuatilia masuala ya utoroshaji fedha
na kufichwa kwenye benki za huko, alisema kuwa wakati shinikizo la
dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na utoroshaji wa
fedha kutoka nchi za Afrika, lakini Serikali ya Tanzania inasuasua juu
ya kupambana na jambo hilo.
Zitto alisema katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari kuwa moja ya njia ya Serikali za nchi maskini kupata
taarifa za kampuni kubwa za kimataifa yanayokwepa kodi ni mfumo wa
kupashana taarifa unaoitwa kwa lugha ya Kiingereza `automatic exchange
of tax information’.
“Kutokana na shinikizo la nchi
mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa `tax havens’ (nchi zinazohifadhi
fedha kwa siri) fedha zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa
taarifa,” alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema).
Alisema kuwa Tanzania mpaka sasa
haijaweka saini na Serikali haijatoa taarifa yoyote kwa umma juu ya
sababu ya kutokufanya hivyo. “Ghana, Afrika Kusini na Nigeria nchi
zinazotegemea sana rasilimali kama Tanzania zimeweka saini mkataba huu
tayari,” aliongeza Zitto.Alisema asilimia 44 ya fedha za kigeni
inazopata Serikali ya Tanzania zinatokana na mauzo ya madini nje.
Kampuni za madini ndizo zinazoongoza kukwepa kodi.
Alisema Tanzania inapoteza jumla ya
Dola 500 milioni (Sh783 milioni) na Dola 1.25 bilioni (Sh2 trilioni) kwa
mwaka kutokana na kampuni kubwa za kimataifa kukwepa kodi.
“Hii ni sawa na kusema Tanzania inapoteza Dola2 milioni (Sh3.1 bilioni) kila siku kwa uporaji huu,” alisema Zitto.
Zitto alisema Serikali lazima ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania inaingia makubaliano ya kupashana taarifa za kikodi.
Jaji Werema agoma kujibu
Alipoulizwa juu ya Tanzania
kutokusaini mikataba ya kimataifa ya kubadilishana taarifa za utoroshaji
fedha na mambo au kodi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick
Werema alisema hawezi kujibu suala hilo.
“Muulize huyo aliyekwambia kuwa
Tanzania haijasaini mikataba ya kubadilishana taarifa za utoroshaji
fedha na masuala ya kodi. Naomba uniache nifanye kazi zangu,” alijibu
Jaji Werema kwa mkato na kukata simu.
Mahojiano kamili na Rais wa Uswisi, soma Mwananchi Jumapili.
*Mada ya rushwa yaibua malumbano Dodoma
*Wagombea wanyoosheana vidole matumizi ya fedha
BAADHI ya wanasiasa wanaotajwa kutaka
kuwania ukuu wa dola mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM
), sasa wanadaiwa kusababisha malumbano makali kando ya semina ya
mafunzo ya utendaji, yanayowahusisha Wenyeviti na Makatibu wa wilaya na
mikoa wa chama hicho, iliyomalizika jana mjini Dodoma.
RAI limedokezwa kuwa malumbano hayo
yametokana na kitendo cha baadhi ya wanasiasa kuitumia semina hiyo kama
njia ya ushawishi kwa kutoa rushwa ili kujijengea mazingira ya kuteuliwa
kuwa wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2015, hali iliyowaibua
baadhi ya makada wa chama hicho ambao wamewanyooshea vidole vigogo hao.
Habari zilizolifikia RAI kutoka ndani
ya semina hiyo iliyohitimishwa jana na Rais Jakaya Kikwete mjini
Dodoma, zimeeleza kuwa baadhi ya wajumbe, waliwashambulia kwa maneno
makali makada wenzao kuwa tamaa yao ya uongozi inayowasukuma kutumia
fedha nyingi kutafuta uungwaji mkono, inakichafua chama.
Mmoja wa wajumbe wa semina hiyo
aliyezungumza na gazeti hili (jina lake tunaliifadhi) alisema kuwa,
yaliibuka malumbano makali wakati mmoja wa mawaziri vijana na kada wa
CCM mwenye ushawishi kwa vijana alipokuwa akiwasilisha mada yake
iliyohusu mwelekeo wa CCM na taswira ya wapiga kura katika uchaguzi mkuu
ujao wa mwaka 2015.
Inaelezwa kuwa katika mada hiyo,
Naibu Waziri huyo kijana alieleza namna CCM kilivyoanza kupoteza
mwelekeo na mvuto kwa wapiga kura kwa sababu ya uwepo wa makundi ya
wanachama wake wanaotumia fedha kusaka uongozi.
Mtoa habari huyo alieleza kuwa kauli
ya waziri huyo ambaye pia amekuwa akitajwa kuendesha mikakati ya chini
kwa chini ya kutafuta uungwaji mkono kwa ajili ya kuwania urais 2015,
iliibua malumbano kando ya ukumbi wa semina na baadhi ya wajumbe
wakimnyooshea kidole kuwa hata yeye anatuhumiwa kutumia fedha katika
harakati zake.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu,
baadhi ya wajumbe walihoji alikopata uhalali wa kuzungumzia jambo hilo
ili hali yeye mwenyewe ameutumia mkutano huo kugawa rushwa ya Sh 50,000
kwa makatibu 50 na wenyeviti 50 wa baadhi ya mikoa na wilaya.
Haikufahamika mara moja waziri huyo
kijana alikotoa fedha hizo, lakini taarifa zaidi kutoka ndani ya semina
hiyo zinaeleza kuwa kuna idadi kubwa ya wapambe wa watu
waliokwishaonyesha nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao, ambao
wamekuwa wakijipitisha kwa wajumbe wa mkutano huo na kuwagawia fedha.
RAI limetajiwa majina ya vigogo
wawili wa CCM wenye asili ya Kanda ya Ziwa ambao wapambe wao wameonekana
wakiwapatia bahasha za kaki baadhi ya wajumbe ambao baada ya kuzifungua
wamekaririwa wakieleza kukuta fedha ndani.
Mmoja wa vigogo hao anatajwa kuwa ni
waziri mwandamizi katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, naye anamtumia
mmoja wa wabunge wa mkoa wake kugawa kiasi cha Sh 200,000 kwa wajumbe
aliokwishawafikia.
Inaelezwa kuwa mpambe huyo wa Waziri
aliibua malalamiko kutoka kwa wajumbe wa Zanzibar, ambao hakuwapatia
fedha na walipomhoji ni kwanini anawabagua katika mgawo huo, alijibu
kuwa hakupewa majina yao lakini watu walio karibu naye wameeleza kuwa
Wazanzibari hawapo kwenye mgao kwa sababu hawana nguvu ya ushawishi
katika vikao vya uteuzi vya wagombea urais.
Mbali na waziri huyo, anatajwa pia
aliyepata kuwa waziri katika moja ya wizara nyeti kabla ya kufanyika kwa
mabadiliko ya baraza la mawaziri, ambayo yalimuacha pembeni kuwa naye
ametuma wapambe wake katika semina hiyo ambao wamekuwa wakiwafikia
wajumbe wa semina hiyo kwa kuwaomba wamuunge mkono katika nia yake ya
kuwania urais mwaka 2015.
Wapambe hao wa mwanasiasa huyo
kijana, ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na pia walikuwa
wabunge katika Bunge lililopita ambao wanawagawia wajumbe wanaowafikia
bahasha zenye Sh 100,000 hadi Sh 150,000 ili kuhakikisha mgombea wao
anaungwa mkono wakati utakapofika.
Jitihada za gazeti hili kumpata
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahiman Kinana kuzungumzia suala hilo,
hazikufanikiwa baada ya simu yake ya kiganjani kuita muda mrefu bila
kupokelewa.