Mh.balozi
akishauriana jambo na mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika wizara ya
mambo ya nje Bi.Mindi Kasiga ambaye atakuwa ndio MC wa shughuli hiyo.
Mh.Balozi
wa Tanzania Marekani na Mexico Liberata Mulamula akizungumzia
maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya muungano ofisini kwake Washington
Dc Jumatano, Aprili 23, 2014.
Mwenyekiti
mwenza wa kamati ya maandalizi afisa ubalozi Suleiman Saleh akijibu
maswali ya mabloger wa DMV,kulia kwake ni Dickson Mkama wa Swahili TV
Mh, balozi akijibu maswali kushoto ni Sunday Shomari na kulia kwa balozi ni Mubelwa Bandio wa Kwanza production.
--
Katika mkutano huo na mablogger wa DMV Mh,Balozi Liberata Mula mula amesema maandalizi sasa yamepamba moto ikiwa ndio count down kuelekea D-day (wakihesabu siku zilizobaki kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya miaka 50 ya muungano wa Tanzania). Mh.balozi ameasa watanzania wa DMV na majimbo ya karibu kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo kwani ni siku ya kihistoria kwa taifa la Tanzania na inafanyika kwa mara ya kwanza Washington Dc.
Katika mkutano huo na mablogger wa DMV Mh,Balozi Liberata Mula mula amesema maandalizi sasa yamepamba moto ikiwa ndio count down kuelekea D-day (wakihesabu siku zilizobaki kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya miaka 50 ya muungano wa Tanzania). Mh.balozi ameasa watanzania wa DMV na majimbo ya karibu kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo kwani ni siku ya kihistoria kwa taifa la Tanzania na inafanyika kwa mara ya kwanza Washington Dc.
Ameeleza
kuwa kila kitu kitu kiko tayari na katika siku hiyo ameeleza
mtiriririko mzima ambapo sherehe zitaanza asubuhi katika ofisi za
ubalozi wa Tanzania Dc ambapo kutakuwa na "Open house " ikiwa na maana
maonyesho ya kuitangaza Tanzania ilikotoka, iliko na inakoelekea ikiwa
ni pamoja na maonyesho ya mitindo , utalii na mavazi ya mtanzania ,
shughuli hiyo itaanza saa 4 asubuhi mpaka saa tisa alasiri.
Na katika hafla hiyo kutakuwa na vyakula vya aina mbali mbali vya
Tanzania kuanzia kifungua kinywa mpaka chakula cha mchana ambapo
kutakuwa na vyakula mbali mbali vya Tanzania kama vile mihogo, maandazi,
kalmati n.k.
vitafunwa
hivyo vipo zaidi ya aina 22, aidha amesema pia kutakuwa na chakula cha
mchana ikiwa utakosa cha asubuhi kama vile pilau, maharage, mihogo ya
Nazi n.k.
Mchana chakula kitapatikana kati ya saa 7 hadi 8 alasiri pia kutakuwa na
vinywaji kutoka Tanzania kama vile Konyagi, bia za Tanzania, Juice na
wine ambavyo tayari vimeshawasili. Vyakula hivi ni bila malipo yeyote
amesisitiza.
Kutakuwa na maonyesho mbali mbali ikiwa ni pamoja na mavazi, mitindo na
michezo ya kuigiza.
Na
baada ya hapo jioni kuanzia saa mbili usiku kutakuwa na hafla rasmi ya
usiku "Tanzania Muungano Night" ambapo wote mnaalikwa bila kukosa na
bila kuchelewa katika ukumbi wa Matnice Events and Conference Center
7925 Central Avenue Capital Heights Md 20743.
Wageni rasmi ni kutoka pande mbili za muungano ambao Mh. Mwigulu Nchemba
(Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa
Zanzibar atakuwepo Mh. Dr.Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa nchi
ofisi ya rais ambaye pia ni
Mwenyekiti
wa baraza la Mapinduzi Zanzibar na watawasili kuanzia Ijumaa hapa
Washington Dc.
Wageni kutoka serikali ya Marekani ni balozi Donald Tate Boum naibu
waziri wa mambo ya nje anayeshughulikia masuala ya Afrika pamoja na
viongozi wa biashara na viongozi wa mabalozi kutoka kila kanda.
Shughuli
ya usiku itaanza saa mbili kamili mpaka Liamba ambayo kutakuwa na
vyakula vya kila aina kwa ajili yako hakuna kiingilio wala malipo ya
chakula ila katika upande wa vinywaji ni mfuko wako tu kunywa unachotaka
alisisitiza balozi.
Kutakuwa na waigizaji, waimbaji , ngonjera , muziki na kila aina ya
burudani na siku ya Jumapili itakamilishwa na kabumbu "Muungano soccer
tournament" kuanzia saa tisa alasiri huko Fairland recreational Park
3928 Green castle Rd, Fairland Md 20866.
Timu
ya Zanzibar Heroes ya DMV ambayo itapambana na Kilimanjaro stars ya DMV
na balozi atafungua mechi hiyo kwa kupiga mpira na ameahidi atafunga
goli , aidha Mh.balozi amesema michezo ni mingi ikiwa ni pamoja na
kuvuta kambi n.k na kuwaomba wakazi wa DMV na familia zao wajitokeze kwa
wingi.
Washindi watapata medali na vikombe aliongeza balozi akisema "hamtatoka
mikono mitupu na nyama choma ni za kutosha sana zitakuwepo zikiongozwa
na wanajumuiya wa DMV wenyewe".