Sunday, October 20, 2013

Al Ahly kuingia uwanjani na matatizo

Al Ahly inaingia katika mechi ya mkondo wa pili wa michuano Klabu Bingwa barani Afrika dhidi Coton Sport mwishoni mwa wiki huku ikikabiliwa na matatizo lukuki.
Timu hiyo sasa itabidi kuwa na wachezaji wake maarufu ambao wamekata tamaa, kutimuliwa kwa kocha na kuchezea katika uwanja usio na mashabiki.
Jambo linaonekana kama ni matukio ya kawaida kwa timu hiyo yenye rekodi ya kunyakua ubingwa wa Afrika mara saba baada ya kutoka sare ya 1 -1 nchini Cameroon wiki mbili zilizopita imekuwa katika hali isiyo ya kuridhisha wiki hii.
Ahly imetoa wachezaji nane wanaochezea timu ya Taifa ya Misri iliyokubali kipigo cha mabao 6 -1 kutoka kwa Ghana katika mechi ya mkondo wa kwanza ya kufuzu kucheza kombe la dunia iliyopigwa siku ya jumanne, na kuondoa matumaini ya Misri kwenda kucheza fainali hizo nchini Brazil mwaka 2014.
Baada ya kuona ndoto ya kucheza kombe la dunia imefifia mchezaji mkongwe anacheza nafasi ya kiungo Mohamed Aboutrika amesema atastaafu soka baada ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika kumalizika.

Arsenal yazidi kutamba

 
Arsenal wakishangilia ushindi
Arsenal wakishangilia ushindi
Ushindi wa Arsenal dhidi ya Norwich umeiwezesha kwendelea kuongoza ligi kuu ya premier ya England.
Mesut Ozil amefunga mabao 2 miongoni mwa 4-1 yaliyofungwa na Arsenal kwenye uwanja wao wa Emerates.
Goli la kwanza limefungwa na Jack Wilshere kwa ustadi mkubwa kunako dakika ya 17 ya mchezo.Mesut Ozil amepiga la pili kunako dakika ya 57 kabla ya Norwich kupata bao lao lililoingizwa na Jonathan Howson dakika 10 baadae.
Aaron Ramsey amepachika goli la 3 la Arsenal kwenye dakika ya 82 na Ozil kufunga kazi dakika 3 kabla ya kipenga cha mwisho kulia.
Kwa ushindi huo Arsenal inaendelea kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 19 baada ya mechi 8 zilizokwisha chezwa.inafwatiwa na Chelsea yenye alama 17 sawa na Liverpool,lakini wanatofautiana kwa magoli.

Moto wazidi kuwa mkali Australia

 
Athari za moto New South Wales, Australia
Serikali ya Australia imetangaza hali ya dharura katika jimbo la New South Wales, ambako wazima moto wanaopambana na moto wa vichakani wanajizatiti kwa hali inayozidi kuwa mbaya.
Hali ya dharura inawapa wakuu idhini ya kulazimisha watu wahame majumbani mwao na kuzima umeme ikihitajika.
Watabiri wa hali ya hewa wanasema joto litazidi na upepo kuzidi kasi na hivo kuupepea huo moto katika siku zijazo.
Mkuu wa kitengo cha wazima moto mashambani katika jimbo la New South Wales, Shane Fitzsimmons, aliwaambia waandishi wa habari kwamba anataraji hali kuzidi kuwa ya hatari.

Msaada wahitajika kitongoji cha Damascus

 
Moadamiyet, kitongoji cha Damascus
Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na msaada wa dharura, , Valerie Amos, ametoa wito mapigano yasitishwe katika kitongoji cha mji mkuu wa Syria, Damascus, ili kuruhusu chakula na madawa kupelekwa.
Alisema ingawa watu maelfu walikihama kitongoje cha Moadamiyet, juma lilopita, hata hivo maelfu bado wamenasa.
Matamshi yake yanafanana na yale ya wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Marekani, ambayo iliitaka Syria iruhusu msaada wa dharura ufikishwe vitongoji - vitongoji vinavyodhibitiwa na wapiganaji na ambavyo vimezingirwa na jeshi la serikali.
Katika tukio jengine, wanaharakati wanasema kuwa wanajeshi kama 16 wameuwawa kwenye mripuko wa bomu lilotegwa kwenye gari katika kitongoji cha Jaramana, ambacho ni kitiifu kwa Rais Assad.

Wahalifu wa DRC hawakupelekwa mahakamani

 
Wanajeshi wa serikali ya Congo
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo unasema unasikitika kuwa watu waliofanya ukatili katika mji wa Minova mwaka jana hawakufikishwa mahakamani.
Umoja wa Mataifa unasema una ushahidi wa kesi 135 za ubakaji pamoja na mauaji na wizi wa ngawira uliofanywa katika eneo la Minova mwezi Novemba mwaka jana.
Ulilishutumu jeshi la Congo kufanya uhalifu huo.
Inaarifiwa maafisa 12 wa jeshi la Congo walisimamishwa kazi kwa muda, lakini Umoja wa Mataifa unasema hakuna aliyefikishwa mahakamani.

Tuesday, October 15, 2013

SHAHIDI AELEZEA JINSI UFOO SARO ALIVYOPIGWA RISASI NA MAMA YAKE KUUWAWA


Kwa mujibu wa ITV tukio lilitokea saa kumi na mbili na nusu nyumbani alipokua akiishi mama mzazi wa mwandishi wa ITV Ufoo ambae ni Anastazia ambapo baada ya taarifa kufika ITV, timu ya ITV  ilifatilia tukio hilo na kushuhudia gari la wagonjwa la Hospitali ya Tumbi Kibaha Pwani ikiwa imembeba Ufoo kumuondoa kwenye hospitali hiyo ili kumuwaisha Muhimbili hospital.

Wakati huo mpaka Ufoo anafikishwa hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha dharura, miili miwili ambayo ni wa mama yake mzazi na mwanaume aliemuua mama kwa risasi na kisha kujiua yeye pia kwa risasi ya kichwa ilikua ikiingizwa kuhifadhiwa.

Shuhuda wa tukio hilo ambae ni mpangaji aliepanga nyumba ya mama yake na Ufoo, Mr Ngowi amesema ‘walikua wanagombana huko ndani na kelele za bastola zinasikika, tukafika tukakuta damu zimetapakaa chini barazani tukamuona na mama amelala chini ndio nikatoa taarifa kituo cha polisi na kukuta Marehemu amemuua mama mkwe na yeye mwenyewe kujiua’


Mwenyekiti mtendaji wa IPP Reginald Mengi alifika hospitali kumjulia hali Ufoo ambapo alisema ‘nimesema na Madaktari ana majeraha lakini hatujui ni mangapi kwa sababu bado wanamfanyia uchunguzi na baadae kidogo atafanyiwa upasuaji, nina imani kwamba Ufoo atarudi kwenye hali yake ya afya njema’

Monday, October 14, 2013

PICHA ZA WAHAMIAJI HARAMU WALIO KAMATWA JANA MKOANI MOROGORO WAKIWA KWENYE GARI LILIBEBA CHOKAA


Wahamiaji haramu wakiwa kituo cha polisi mkoani morogoro mara baada ya kukamatwajana wakisafirishwa


Mmoja wa wahamiaji haramu akishushwa katika gari la mizigo lillokuwa limebeba shehena ya chokaa lililokuwa likitokea mkoa wa tanga na kukamatwa jana mkoani morogoro