Monday, July 8, 2013
FAMILIA YA MANDELA WASHIKANA UGONI SOUTH AFRICA
*Mandla amtuhumu Mbuso kuzaa na mkewe
CHIFU Zwelivelile Mandlesizwe Dilubhunga ‘Mandla’ Mandela (39), ambaye ni mjukuu mkubwa wa kiume wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amemtuhumu mdogo wake, Mbuso Mandela (22) kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.
Tuhuma hizo nzito ndani ya familia ya Mandela, zimeibuliwa na Mandla kwa kumtaja jina moja kwa moja Mbuso kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake wa pili, Anais Grimaud, ambaye alimpa ujauzito. Mandla na Mbuso ni watoto wa Marehemu Makgatho Mandela ambaye ni mtoto wa kiume wa Mandela kwa mkewe wa kwanza, Marehemu Evelyne Maso.
Watu walio karibu na familia ya Mandela, wamepata kukaririwa na vyombo vya habari vya nchini hapa wakieleza kuwa, Mandla amekuwa akilalamika mara nyingi kuwa mke wake ambaye wameshatalikiana, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa ndugu zake, lakini hakuwahi kumtaja kwa jina.
Katika malalamiko yake hayo, Mandla alikaririwa akieleza kuwa, ndugu yake alimpa mimba mke wake na kuzaa naye mtoto mmoja jambo ambalo wanafamilia wamelifumbia macho wakati wanajua alitendewa vibaya.
Alhamisi wiki iliyopita, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Mvezo, Eastern Cape, baada ya kushindwa kesi aliyokuwa amefunguliwa na shangazi yake, Makaziwe Mandela ya kuvamia eneo la makaburi usiku na kuiba mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela, Mandla alisema anashangazwa na watu wanaojiita wanafamilia ya Mandela kudai wanataka amani ndani ya ukoo wakati malalamiko yake hawajawahi kuyashughulikia.
Katika mkutano wake huo, Mandla alisema mke wake aliyemuita ni mzuri, Anais, ambaye ni raia wa Ufaransa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mdogo wake wa damu aliyemtaja jina kwa mara ya kwanza, kuwa ni Mbuso.
Alisema kwamba, alipopata taarifa hizo, alishtuka na kuumia na alimtaja mtoto ambaye mke wake alizaa na mdogo wake Mbuso kuwa anaitwa Nkosi Qheya II Zanethemba Mandela.
Mandla alisema alilazimika kuachana na mkewe huyo aliyemuoa mwaka 2010 na kwamba aliamua kumbadili jina mtoto aliyezaa na Mbuso na kumuita Nkosikazi Nobubule, kabla hajaondoka kwenye makazi ya Mandla na kurejea kwao Ufaransa.
Tuhuma hizi zilizotolewa na Mandla juzi kwa mara ya kwanza, ziliripotiwa na Gazeti la Sunday Sun la Afrika Kusini mwaka jana na kuibuka tena wiki iliyopita.
Taarifa hizo, zimezidi kuipa nguvu hofu ya baadhi ya watu wanaofuatilia mtafaruku wa ndani ya familia ya Mandela ambaye kwa sasa anapigania uhai akiwa hospitalini.
Kwa zaidi ya wiki mbili sasa, familia ya Mandela imekuwa katika mnyukano wa kugombea uhalali wa eneo linalostahili kuwa maalumu kwa ajili ya kuzika marehemu wa familia hiyo baada ya Mandla kuhamisha mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela, waliokuwa wamezikwa katika nyumba yake iliyoko kijijini Qunu na kwenda kuwazika kwenye makazi yake ya kichifu ya Mzove.
Mahakama Kuu ya Mthatha ya Jimbo la Eastern Cape ilimtia hatiani Mandla aliyekuwa akishitakiwa na wanafamilia 16, ambapo ilimuamuru arejeshe mabaki ya miili hiyo Qunu.
Wakati hali ikiwa hivyo kwa familia yake, Mandela bado yuko mahututi hospitali mjini Pretoria na hakuna taariza zozote za mabadiliko ya afya yake.
MASKINI:MWANAFUNZI AJILIPUA NA MAFUTA YA PETROL
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.
Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua.
“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.
“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).
Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.
PICHA ZA MPAMBANO WA NGUMI WA HALIMA MDEE NA JACK WOLPER
Jana katika tamasha la matumaini Jackline Wolper na Halima Mdee walizipiga ....hapakupatikana mshindi baada ya kutoka Droo
WANAWAKE WAWILI WAMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA AFRIKA KUSINI WAKITOKEA TANZANI
Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.
Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.
“When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa.
Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller.
Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini.
Wednesday, July 3, 2013
Mabilionea Tanzania wakutana na Obama
‘Tumezungumza mengi na Obama, ila ulikuwa mkutano wa ndani na mrefu, tumezungumza mengi kwa kweli.’
Reginald Mengi,
Mkurugenzi Mtendaji wa IPP
Kwa ufupi
Mabilionea hao ni kati ya wale waliotajwa katika jarida la Ventures Afrika linalozungumzia masuala ya uchumi wa Afrika.
Dar es Salaam. Rais wa Marekani, Barack Obama
juzi alikutana na kundi la wafanyabiashara 20 wakubwa barani Afrika
wakiwemo Watanzania watatu ambao utajiri wao ulitajwa katika jarida la
Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika,
kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.
Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani alikutana
na wafanyabiashara hao juzi jioni katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro na
kufanya nao mazungumzo kwa saa 1:23, huku waandishi wa habari wakipewa
ruhusa ya kupiga picha tu.
Jarida hilo lililotolewa mwaka jana liliwataja
wafanyabiashara hao kuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa
Group, Said Salim Bakhresa, Gulam Dewji, Rostam Aziz, Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni ya IPP, Reginald Mengi na Mwanzilishi na Mwenyekiti
Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group, Ali Mufuruki.
Hata hivyo, juzi wafanyabiashara waliokuwa katika orodha ya kukutana na Rais Obama ni Bakhressa, Mengi na Mufuruki.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa
anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni
sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye
utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni).
Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki
kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi
(Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110
milioni).
Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Rais
Obama alizungumza tena na wafanyabiashara wengine 170 kutoka Afrika na
Tanzania kwa dakika 17, lakini hakuweka wazi walichozungumza na
wafanyabiashara hao 20.
Wafanyabiashara wengine waliokuwepo katika kikao
hicho ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Africa Finance
Corporation, Andwer Alli, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo Afrika,
Don Kaberuka..
Wengine ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera, Mwenyekiti wa Econet, Strive
Masiyiwa, Mkurugenzi Mkuu wa Equity Benki, James Mwangi, Mwenyekiti wa
Export Trading Group, Mahesh Patel.
Mkurugenzi Mkuu wa General Electric, Jay Ireland,
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Harith, Tshepo Mahloele, Mwenyekiti wa
Heirs Holdings, Tony Elumelu.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Microsoft Afrika, Ali
Faramawy, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Prudential Plc, Tidjane
Thiam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Peter Sands,
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Symbion Power, Paul Hinks, Mwanzilishi na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanjet, Susan Mashibe pamoja na
Mwenyekiti wa Benki ya United Afrika, Phillips Oduoza.
Katika meza kuu Obama alikuwa amekaa pamoja na Mashibe, Mahloele, Masiyiwa na Kalumbu.
MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT JIJINI MBEYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 BAADA YA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI
Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemtia hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).
Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shitaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana na mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.
Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimharibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani , hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha.
Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kuhusu kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake..
LIMO YA OBAMA INAWEZA KWENDA 97KM TU KWA SAA AT MAXIMUM
Walioona msafara wa obama wataona namna msafara ulipita kwa speed ya kawaida sana tofauti na ile speed tuliyozoea anapopita JK, our president normally huwa ana cruise at an average of 120kmh.
Ile speed ikanifanya nitafute habari zaidi, niliyoyaona yamenishangaza, kumbe
- Maximum speed ya limo ya
obama ni 60mph tu, sawasawa na kilimita kama 97 kwa saa. hii gari haina
ujanja wa kwenda hata 100km kwa saa, hata boda boda inaweza kwenda
speed kuliko hii gari
- ina uzito unaokadiria kukaribia tani 9
- matumizi ya mafuta ni 8mpg, kwa
lugha ingine inahitahi lita 35.31 ili kutembea kilomita 100, hii ni sawa
na lita 1 kwa kila kilomita 2.8
- vioo vyote havifunguki isipokua pale kwa dereva kwa mbele. gari iko 100% sealed
- Vioo vya dirishani vina thickness ya inchi 5 wakati milango ni nchi 8.
- kutokana na unene wa madirisha
na milango, obama hawezi kusikia chochote kinachoendelea nnje, spika
zimewekwa ili kunasa sauti za nje
- gari ina night vision kamera zinazomuwezesha dereva kuendesha usiku bila hata kuwasha taa
Subscribe to:
Posts (Atom)








