Sunday, October 13, 2013

Nu Joint: Tema Mate Tuwachape - Madee

Mkono mwingine kutoka kwa makochali, ni Madee kwa mbali unamsikia Raymond, pini linaitwa Tema Mate Tuwachape.

Ni ngoma ambayo style yake inaitwa "Kwata" ikiwa ni mchanganyiko wa kwaito ya South Africa na Takeu ya Kenya" amesema Madee.

UFOO SARO WA ITV APIGWA RISASI, MAMA YAKE AUWAWA..ALIYE WAPIGA NI MCHUMBA WAKE NAE AJIUA


Alfajiri  ya  leo, mtangazaji  wa  ITV   anayejulikana  kwa  jina  la  Ufoo Saro  amejeruhiwa  vibaya  kwa  kupigwa  risasi  na  mchumba  wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua.

Akizungumza na mpekuzi wetu,  kamanda Wambura  ambaye  ni kamanda  wa polisi wa  mkoa wa kipolisi wa kinondoni  amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.

Kamanda wambura amedai  kuwa mwanaume  aliyetenda  mauaji  hayo ni  mchumba  wake  na  alikuwa anafanya  kazi  katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika  kitengo alichokuwa  akifanyia  kazi.

Kwa  mujibu  wa  Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili  awasuluhishe

Baada  ya  usuluhishi  kuanza  na  kuonekana  kuwa  tatizo  liko  kwa  mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa  na  mazoea  ya  kumtetea mwanae   na  ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro risasi ya kichwa na kumuua papo hapo....


Alipomuua  mama  huyo, mwanaume huyo  alimpiga Ufoo Saro risasi mbili , moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.

Friday, October 11, 2013

NGASSA ARUDI AZAM, AUNGANA NA MWAIKIMBA



Na Khatimu Naheka
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa ameikumbuka timu yake ya zamani ya Azam FC baada ya kuonekana akiwa kwenye Uwanja wa Chamazi Complex nje ya jiji la Dar es Salaam.
Ngassa, ambaye awali aliuzwa na Yanga kwenda Azam FC kwa kitita cha pauni milioni 98, miaka mitatu iliyopita kabla ya kurudi msimu huu, juzi alitua kwenye Uwanja wa Chamazi na kushuhudia mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji na Mgambo Shooting.
Ngassa aliyeondoka Azam FC kwa mgogoro huku timu hiyo ikimpeleka Simba, alikuwa kivutio na wengi walianza kuonyeshana alipokuwa amekaa jukwaani.
Baada ya kufika uwanjani hapo, moja kwa moja Ngassa alikwenda kukaa alipokuwa amekaa mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba waliyewahi kukipiga pamoja Jangwani.
Mara baada ya mechi hiyo, kiungo huyo aliyerudi kwa kasi katika Klabu ya Yanga, kwa kuifungia bao moja mpaka sasa, alisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na kuondoka zake.
Ngassa alipoulizwa sababu za kwenda uwanjani hapo alisema kwa ufupi: “Nimekuja kutembea tu.”

Tayari Ngassa yupo mjini Bukoba kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar, kesho.

TB JOSHUA AITABIRIA MAKUBWA TEAM YA ARSENAL


 Katika Profile yake ya Tweeter Mchungaji maarufu wa Nigeria TB Joshua aliandika haya 

WAZIRI MKUU PINDA AMUONYA VIKALI MAGUFULI


*Asema uamuzi wake haukushirikisha wizara nyingine

*Adai wadau walipaswa kupewa muda zaidi, aonya rushwa

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amemuonya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kwa mara nyingine tena kuacha tabia ya kufanya uamuzi wa jambo lolote bila kushirikisha pande zinazohusika.

Mbali ya karipio hilo, Waziri Mkuu amewataka viongozi wengine wa Serikali, kuepuka mfumo usio shirikishi katika uamuzi wao kwa kuwa unasababisha migogoro ndani ya jamii na usumbufu kwa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mgomo wa wasafirishaji wa mizigo na abiria ulioanza Oktoba 5, mwaka huu, Pinda alisema Serikali imeamua kurejesha kwa muda wa mwezi mmoja asilimia tano ya uzito wa mizigo uliozidi kwenye mizani.


Alisema hatua zilizochukuliwa na Dk. Magufuli kufuta vifungu vilivyokuwa vikiruhusu asilimia tano zilifuata sheria, lakini tatizo lililojitokeza ni kutoshirikisha pande zinazohusika ili kushauriana na kupata uamuzi wa pamoja.

Alisema mbali ya kutoshirikisha pande hizo, uamuzi wa Dk. Magufuli ulikuwa wa ghafla kwa wasafirishaji kitendo ambacho kimewapa wakati mgumu wa utekelezaji, kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wameingia mikataba na wateja wao.

“Chimbuko la mgogoro huu, ni tangazo la Dk. Magufuli alilotoa Oktoba mosi, mwaka huu la kuondoa ofa ya asilimia ya uzito uliozidi, baada ya uamuzi huo wadau wa usafirishaji wa malori na mabasi waliingia kwenye mgomo na kulalamikia hatua hiyo.

“Kutokana na mgogoro huu, nililazimika kukutana na Dk. Magufuli, baadhi ya mawaziri wa wizara zenye uhusiano na masuala haya, wanasheria na wataalamu wa masuala ya usafiri na uchumi.

“Kilichoongeza mgogoro ni tafsiri ya vifungu vya sheria na kwenye kanuni ya 7 (2) na 7(3) ambacho kinaeleza wasafirishaji wa magari yenye uzito uliozidi, lakini upo ndani ya asilimia tano ya uzito unaokubaliwa kisheria, wanatakiwa kupunguza mzigo, kupinga na iwapo watashindwa kutekeleza, watatakiwa kulipia mara nne ya tozo za kawaida.

“Sasa suala la asilimia tano, lilitokana na ombi la wadau wa usafirishaji kwa aliyekuwa waziri wa Ujenzi miaka ya nyuma na halikuwa sheria kamili, ndio maana limeondolewa baada ya kuonekana linatumiwa vibaya.


“Nakubaliana na Dk. Magufuli, wapo baadhi ya wasafirishaji ni wakorofi na hawataki kufuata sheria…ndio maana walifanya mazoea ingawa wapo wengine wazuri na hao nawapongeza sana kutii sheria.
-Mtanzania

YANGA YATAMBA "TUTAIFUNGA SIMBA KIRAHISI KAMA KUMSUKUMA MLEVI TAREHE 20 OCT"


KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Ernest Brandts, amesema kuifunga Simba katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom itakayochezwa Oktoba 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ni kazi rahisi. Brandts amewatoa hofu viongozi na mashabiki wa Yanga, huku akitamba kupata ushindi dhidi ya mahasimu wao Simba. 

Akizungumza na RAI jana, Brandts alisema Simba hawamtishi kwa kuwa ana kikosi bora ambacho kina kila sababu ya kushinda mechi hiyo.

Alisema amekuwa akiifuatilia Simba mara nyingi inapocheza mechi na hakuna ushindani ambao umekuwa ukionyeshwa na wachezaji wa timu hiyo, licha ya kupata ushindi katika mechi zake.

“Simba hawana kiwango kikubwa, wanabebwa na mabao ambayo kwa bahati wamekuwa wakifunga, kikosi changu mimi ni bora, wachezaji wangu wana nguvu za kutosha na uwezo zaidi kuhakikisha tunashinda,” alisema.


Yanga tayari imewasili Bukoba kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba

HAFRA FUPI YA KUWAAGA BUKOBA VETERANI WANAOKWENDA ARUSHA KUSHIRIKI BONANZA LA KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE, IKIFANYIKA VIWANJA VYA IBRACADABRAA TAKE AWAY.


 Mwenyekiti wa bukoba veterani Ernest nyambo akimshukuru  bw Ibra (kulia) alieandaa hafra hii jioni ya leo kuagana na wachezaji wenzake wanaoelekea Arusha. Mashindano hayo yatafanyika katika uwanja wa shekhe amri abedi,yatakutanisha timu kutoka mikoa ya Dar-es-salaam,mwanza ,kigoma  na wenyeji kitambi noma ya mjini arusha,pia itakuwepo na michezo mingine kwa ajili ya kumuenzi baba wa taifa la tanzania,Mwenyekiti ametumia nafasi hii kuwashukuru wadau mbalimbali wa bukoba walishiriki kwa hali na mali na kufanikisha safari.        kingmuddy  akipata kitu roho inapenda
                                                                 dada wa veterani
                                                    super mkude kwenye mstari
                                                              nyama choma kama kawaida
                                               weka cha kutosha mwili siunauona huu
                                                                    salumu bonge kama kawaida
                                       veterani,mtensa, super mkude na jamco wakipata msosi
                                                                  ni full makulaji
 jamco akiwa na bw Ibrah alieandaa hafra hii,ongera ibra kwa uzalendo na mapenzi ya kweli kwa wenzako
                             hafra hii ilifanyika barabara ya uganda  katika mgahawa wa Ibracadabraa
                                   
BUKOBA FLOW ZONE IKISHILIKIANA NA BUKOBA STARLINK TUNAWATAKIA SAFARI NJEMA NA MUNGU AWATANGULIE.